Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Ndugu Tixon Nzunda, ameipongeza Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa utekelezaji mzuri wa miradi katika sekta ya elimu kwani majengo yote aliyoyakagua yanaendana na thamani ya fedha iliyotolewa
Pongezi hizo alizitoa jana tarehe 28.07.2019 alipokuwa katika ziara ya kikazi katika Manispaa ya Ilemela kwa lengo la kukagua utekelezaji/ukamilishaji wa ujenzi wa miundombinu katika sekta ya elimu Msingi na Sekondari kupitia fedha zilizotolewa na OR-TAMISEMI kwa ajili ya ukamlishaji wa maboma kattika shule za sekondari pamoja na fedha za EPFR (fedha zinazotolewa kulingana na matokeo).
Ndugu Nzunda alisema kuwa amefurahishwa na namna ambavyo thamani ya fedha inaonekana katika majengo yaliyyojengwa kupitia fedha iliyotolewa na serikali.Alitoa kauli hiyo alipokuwa akikagua ujenzi wa madarasa na bweni la wasichana katika shule ya sekondari ya Buswelu na kuwataka wakurugenzi wengine kuiga mfano huo hasa katika kuhakikisha wanajenga mabweni ya wasichana katika shule za sekondari.
Aidha Ndugu Nzunda akiwa katika ziara hiyo aliweza pia kuongea na walimu na wanafunzi na kuwapongeza walimu kwa juhudi wanayoionesha katika ufundishaji huku akiwataka wanafunzi kusoma kwa bidii ili waweze kufaulu lengo ikiwa ni kurudisha heshima katika shule za umma.Huku akiwataka wanafunzi kuhakikisha wanasoma kwa bidii na kuwa na nidhamu kwani ndio msingi wa mafanikio.
Aliongeza kwa kusisitiza kuwa, kila mwalimu afundishe masomo anayotakiwa kufundisha pamoja na kuhakikisha wanaongeza viwango vya ufaulu. Pia aliwasihi walimu kufanya kazi kwa upendo na kushirikiana huku akiwakumbusha kufanya shughuli za uwekezaji ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Sambamba na hayo amewashukuru walimu kwa kutokumwangusha kwa kufanya matumizi mazuri ya fedha katika ujenzi wa madarasa hayo na kuwataka kuhakikisha wanayatunza hayo majengo ili yaweze kudumu kwa muda mrefu ili vizazi vingine navyo vije vitumie.
Pamoja na hayo amewaagiza viongozi wa sekta ya elimu kuanzia ngazi ya Mkoa,Wilaya pamoja na waratibu elimu kata kuhakikisha kuwa wanasimamia utekelezaji wa mtaala wa elimu pamoja na kutambua kazi nzuri zinazofanywa na walimu.
Nae Mkurugenzi John Wanga akipokea pongezi hizo amemuahidi Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI kuwa atatekeleza yale yote aliyoyaagiza kwa kuhakikisha kuendelea kusimamia kikamilifu sekta ya elimu pamoja na sekta zingine na pia alimshukuru kwa kujitolea kwake kuwa mlezi wa shule ya Sekondari ya Buswelu.
Halmashauri ya Manispaa ya ilemela katika mwaka 2019, upande wa Elimu msingi ilipokea fedha za EP4R kwa mwaka 2019 kiasi cha Tsh.175,00,000.00 kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba 14 va madarasa huku kwa upande wa elimu sekondari kwa mwaka 2018/2019 ilipokea kiasi cha Tsh. 125,000,000 kwa ajili ya ukamillishaji wa maboma kumi ya vyumba vya madarasa katika shule tano ambazo ni Buswelu,Nyasaka,Nyamanoro,Bujingwa na Kisundi.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.