Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela imepokea jumla ya vitabu vya kiada 23, 496 vyenye thamani ya Tsh Milioni 47.8 kwa ajili ya shule za msingi na sekondari kutoka serikali kuu kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET).
Kupokelewa kwa vitabu hivi kunaenda kuboresha mazingira ya kujifunza na kujifunzia pamoja na kuinua taaluma , kujengea wanafunzi uwezo wa kitaaluma ujuzi na maarifa hali inayopelekea kufikia uwiano wa kitabu kimoja kwa wanafunzi watatu (1:3) kwa shule za msingi na wastani wa uwiano wa kitabu kimoja kwa wanafunzi wawili (1:2) kwa shule za sekondari ambapo lengo kuu la serikali ni kufikia uwiano wa kitabu kimoja kwa mwanafunzi mmoja (1:1).
Kati ya vitabu hivyo vilivyopokelewa, vitabu 5786 vyenye thamani ya Tsh. Milioni 6.56 ni kwa ajili ya shule za msingi ni, vitabu 15249 vyenye thamani ya Tsh. Milioni 33.6 kwa shule za sekondari kwa ajili ya kidato cha kwanza hadi cha tatu, na vitabu 2461 kwa ajili ya wanafunzi wa kidato cha tano na sita vya thamani ya Tsh milioni 7.7
Kwa nyakati tofauti Ndugu Sylvester Mrimi ambae ni mkuu wa divisheni ya Elimu Sekondari na Bi hellen John ambae ni Afisa Elimu vifaa na takwimu elimu msingi kwa niaba ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela wameishukuru serikali ya Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa jitihada zote zinazoendelea katika kuboresha mazingira ya kujifunza na kufundishia.
Pamoja na hayo wameahidi kusimamia matumizi ya vitabu hivi ili viweze kuendelea kutumika kwa malengo yaliyokusudiwa kwa faida ya Taifa la Tanzania
Kwa upande wa shule za msingi vitabu vilivyopokelewa ni vya masomo ya hesabu, kuandika, afya na mazingira, uraia na sayansi, na kwa shule za sekondari kidato cha kwanza hadi kidato cha tatu vitabu vilivyopokelewa ni vya somo la hesabu, fizikia na masomo ya kompyuta ambapo kwa upande kidato cha tano na sita vitabu vilivyopokelewa ni pamoja na vitabu vya hesabu, baiolojia, kemia,fizikia na Kiswahili
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.