Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela imepokea jumla ya vitabu 30,364 vyenye thamani ya Tshs. 118,149,702 kutoka Serikali Kuu kupitia Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) lengo ikiwa ni kukamilisha uwiano wa kitabu kimoja kwa mwanafunzi mmoja .
Kufuatia mapokezi ya vitabu hivyo, Afisa Elimu divisheni ya Sekondari Mwalimu Sylvester Mlimi ametoa maelekezo kwa wakuu wa shule wote kuhakikisha wanaweka utaratibu mzuri ili vitabu vitumike kwa wanafunzi wote kuanzia jumatatu na sio kutunza vitabu kwenye mabox.
Sambamba na hilo amesema kuwa Divisheni ya Elimu sekondari imeandaa timu ya kufuatilia kila shule kujionea jinsi vitabu hivyo vinavyotumika kwa wanafunzi kwa lengo la kuinua taaluma.
Mwalimu Sostenes Sombi Mwalimu ws Taaluma katika Shule ya sekondari Bujingwa ameshukuru kwa msaada huu na kusema kuwa kupitia vitabu hivi vitawasaidia katika kujifunzia na kujifunza huku akitoa ombi la vitabu kwa masomo mengine.
Nae Mwalimu Zitta Chambo ambae Mwandamizi taaluma katika Shule ya Sekondari Angeline Mabula mbali na kuishukuru Serikali ya awamu ya sita amesema kuwa vitabu hivi vitawasaidia wanafunzi kujiandaa kabla ya kipindi na baada ya vipindi pamoja na kuwajengea uwezo wa kujiamini juu ya masomo yao na kuwahamasisha watoto kupendelea masomo haya ya sayansi huku nae akitoa ombi kwa masomo mengine pia wapatiwe vitabu.
Vitabu vilivyotolewa ni vya masomo ya Hisabati,Bailojia,Kemia na fizikia kwa wanafunzi wa kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne kwa shule za serikali 32 katika Manispaa ya Ilemela
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.