Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, Mhe Hassan Masala amekabidhiwa msaada wa zaidi ya shilingi milioni 16 kutoka bank ya NMB .
Msaada huo umejumuisha madawati 100 ambayo yamegharimu fedha kiasi cha Shilingi milioni tisa , na vifaa tiba vilivyogharimu takriban shilingi milioni 7.82.
Akikabidhi misaada hiyo Ndugu Baraka Ladislaus, Meneja wa NMB kanda ya ziwa amesema kuwa NMB inatambua jitihada kubws zs serikali hivyo wao kama wadau wa maendeleo wanao wajibu wa kuhakikisha jamii inayowazunguka inafaidika kutokana na faida tunazopata.
"Benki ya NMB itaendelea kuunga mkono juhudi za wadau wake wakubwa katika kuhakikisha kuwa changamoto za jamii zinapatiwa ufumbuzi kwatika kuboresha huduma za jamii", amesema Ndugu Baraka
Mhe.Hassan Masala akipokea msaada huo ameushukuru uongozi wa NMB kwa namna ambavyo wamekuwa wakishiriki katika masuala mbalimbali ya maendeleo Wilayani Ilemela,huku akitoa rai kwa watendaji kuhakikisha vifaa hivi vinatunzwa.
"Vifaa hivi vitunzwe haitapendeza kukuta vinatumika kwa matumizi ambayo hayakukusudiea kwani wahitaji ni wengi na sisi tumepewa heshima kubwa kupatiwa vifaa hivi" aliongeza Mhe Masala.
Nae Mhe Renatus Mulunga ambae ni Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemela pamoja na kushukuru kwa msaada huo ameahidi kuwa upungufu wa madawati kwa sasa utakamilishwa kupitia fedha za mapato ya ndani.
Asteria fredrick ni mwanafunzi kutoka Buswelu Shule ya Msingi ameishukuru NMB kwa msaada wa madawati kwani utawasaidia wanafunzi katika kusoma vizuri.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.