Katibu tawala wa Wilaya ya Ilemela Adv.Mariam Msengi kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe.Hassan Masala amepokea jumla miche ya miti 2500 kutoka kwa mdau wa maendeleo taasisi isiyo ya kiserikali inayotoa huduma mbalimbali za ndege VIA AVIATION Mwanza.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya mapokezi hayo katika shule ya sekondari Kisenga Adv.Msengi amesema Wilaya ya Ilemela inao mpango wa kupanda miti 120,000 kwa mwaka huu 2024 ambapo hadi sasa jumla ya miti 26,000 sawa na 22% imekwisha pandwa maeneo mbalimbali ndani ya Wilaya hiyo.
"Tunashukuru sana kwa miche hii ya miti kwani inaonyesha tupo pamoja na serikali ya awamu ya sita kwa kuunga mkono juhudi za Mhe.Rais za mapambano dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi na utunzaji wa mazingira kwa ujumla wake.Lengo letu ni kutengeneza Ilemela ya kijani."
Adv.Msengi amewataka wakuu wa shule na walimu wakuu wote maeneo yote miti inakoenda kuigawa kwa wanafunzi ambao watawasimamia kila mmoja kuhakikisha mti wake unakuwa vizuri.
Aidha Meneja miradi wa taasisi hiyo Bi.Shose Lyimo ametoa taarifa ya utendaji kazi wao huku akianisha huduma za ndege wanazotoa ikiwemo "flight clearances na private lounge".
Bi. Lyimo amesema ni utaratibu wao kuhamasisha jamii juu ya utunzaji wa mazingira na wanatambua juhudi za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt Samia Suluhu katika sekta ya utunzaji wa mazingira.
" Sisi tunatoa huduma za ndege lakini ni jukumu letu pia kushirikiana na jamii katika shughuli mbalimbali za kimaendeleo."amesema Shose.
Nae Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela ndugu Recipisius Maghembe amewapongeza taasisi hiyo kwa kazi nzuri wanazofanya za kusaidia jamii huku akiwasihi wakuu wa taasisi miti hiyo inakogawiwa kuitunza vyema kwa manufaa ya jamii nzima.
"Tuachane na sababu nyingi nyingi za miti kutokukuwa,miti hii ikasimamiwe vizuri na kulindwa na uwezekano wa yote kukuwa upo." Msafiri Magesa Uthibiti ubora wa shule Manispaa ya Ilemela.
Hashim Cosmas ni mwanafunzi katika shule ya sekondari Kisenga yeye anatoa shukrani kwa wadau wa VIA AVIATION kwa kuwakumbuka katika uboreshaji wa mazingira ya shule kwa kupewa miti hiyo.
"Miti hii ikikua italeta vivuli hapa shuleni na mingine itatupatia matunda na kuleta mandhari ya kuvutia."
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.