Mhe.CPA Amos Makalla Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ameipongeza Manispaa ya Ilemela kwa kupata hati safi katika kipindi cha mwaka wa fedha 2021/2022, ikiwa ni mara tatu mfululizo kuanzia mwaka wa fedha 2019/2020, 2020/2021 na 2021/2022.amezitoa pongezi hizo katika Mkutano maalum wa baraza la madiwani kwa ajili ya kujadili utekelezaji wa hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali
Pamoja na pongezi hizo amesema kuwa wananchi wanafuatilia sana utendaji wa Halmashauri pamoja na taarifa mbalimbali, hivyo kuwa na hati safi kunawajengea imani kubwa wananchi.
Aidha Mhe. Makalla ameishauri Menejimenti ya Ilemela kuhakikisha inashirikiana na ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) ili kuendelea kuzipunguza hoja ambazo sio za lazima.
“Ushauri wangu ili kuendelea kupunguza hoja ambazo sio za lazima menejimenti ishirikane na CAG katika hatua zote za ukaguzi naamini kwa hili hoja zitapungua”Amesema CPA Makalla
Sambamba na hilo amewataka Madiwani kusimamia kidete maslahi mapana ya wananchi kwa kufanyia kazi taarifa ya mkaguzi wa ndani kila anapoiwasilisha hii itasaidia kupunguza hoja.
Diwani kutoka kata ya Pasiansi Mhe. Rose Mayunga akichangia ameshauri wataalam kuhakikisha wanatunza vielelezo vyote ili kuepusha hoja na mwisho wa siku Ilemela iwe na hoja ambazo zinafungwa, alishauri.
Mhe. Manusura Lusigaliye Naibu Meya wa Manispaa ya Ilemela akihitimisha kikao hicho pamoja na kumshukuru Mkuu wa Mkoa kwa namna ameendesha kikao lakini pia amemuahidi kuwa Baraza la Madiwani kwa kushirikiana na watalaam watafanyia kazi maelekezo yote ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa hoja zilizobakia zinafungwa.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.