Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa kushirikiana na wananchi wake imeendelea kushirikiana katika zoezi zima la kuboresha miundombinu ya shule za msingi.
Uboreshaji wa miundombinu ya shule hizi unafuatiwa na upungufu wa madarasa ,upungufu wa matundu ya vyoo, adha ya watoto kutembea umbali mrefu kufika shuleni ambayo yamesababiswha na ongezeko la wanafunzi.
Shule ya Msingi Bugogwa ni moja ya shule ambazo zimekuwa zikikumbwa na changamoto hizo hali iliyopelekea kuanzishwa kwa ujenzi wa shule ya msingi Bugogwa B.
Ujenzi wa shule ya Msingi Bugogwa B katika eneo la Kayenze ndogo ulianza Agosti 2016 kwa nguvu ya wananchi kwa kushirikiana na Mh. Diwani wa kata hiyo pamoja na Mbunge wa jimbo la Ilemela. Aidha, shule hii ilipokea jumla ya shilingi 66,600,000/= (pesa za lipa kulingana na ufanisi-EP4R).
Nayo Manispaa ya Ilemela chini ya usimamizi wa Mkurugenzi John Wanga imeshiriki kikamilifu katika utekelezaji wa mradi huu kwa kutoa wataalamu wa uhandisi majengo na idara ya elimu kwa muda wote wa utekelezaji mradi hali ambayo imepelekea mradi kuendelea bila kusimama.
Mradi huu hadi kukamilika unatarajiwa kugharimu takribani kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 130,000,000 ambapo hadi sasa umegharimu kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 68,943,000/ = ambapo Tsh. 3,980,000/= ni thamani ya nguvu za wananchi, Tsh. 58,953,000/= ni fedha toka serikali Kuu, Tsh. 5,640,000/= ni mchango toka ofisi ya Mh. Mbunge (tofali 5000 na mifuko 40 ya saruji) na vifaa vyenye thamani ya Tsh. 370,000/= ambavyo vimetolewa na diwani wa kata hiyo Mhe William Mashamba.
Uboreshaji wa miundombinu ya shule za msingi katika Manispaa ya Ilemela unaendelea katika shule mbalimbali zikiwemo Isenga, Juhudi, Buhila, Kilabela, Isanzu Lukobe, Pasiansi na Ilemela.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.