Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela itaendelea kuinua ubora wa Elimu kwa kushirikiana na wadau wote wa Elimu ili kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Hayo yamesemwa na Afisa Elimu ya watu wazima wa manispaa ya Ilemela, Recipitius Magembe wakati wa maadhimisho ya wiki ya Elimu ya watu wazima.
Magembe alisema ni jukumu la kila mwenye dhamana ya elimu kuviendeleza vikundi kiujuzi na maarifa chini ya mpango wa uwio kati ya Elimu na Jamii(Memkwa) wafanye shughuli walizoziamua kama vile ushonaji,Ujasiliamali na ufugaji.
Mgeni rasmi katika maadhimisho hayo mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe. Hassan Masala amesema Elimu ya watu wazima pia inatoa nafasi kwa watu kujiendeleza kutoka hatua ya chini kabisa kielimu hadi elimu ya juu kupitia program zake mbali mbali nje ya mfumo rasmi mfano Mpango wa Elimu kwa waliokosa(Memkwa),Elimu masafa na Elimu malumu kwa wanafunzi na watu wazima wenye mahitaji malumu ya ufundi stadi.
“WanaIlemela sisi ni manispaa ,napenda wote twende pamoja hatuna sababu ya kuwaacha wenzetu nyuma kwa kutokujua kusoma na kuandika”amesema
Manispaa ya Ilemela inayo walimu wawezeshi 20 katika vituo vya elimu ya watu wazima.
Jumla ya wanafunzi 79 wamehitimu elimu ya msingi kwa watu wazima katika mwaka 2021 ambapo kundi hilo linatarajiwa kuingia kidato cha kwanza 2022.
“Wanafunzi 106 wamesajiliwa kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne na tunaamini watafanya vizuri”amesema Maghembe.
Akihitimisha maadhimisho hayo Mkuu wa Wiaya ya Ilemela,Hasan Masala alisisitiza kuwa ni jukumu la kila mmoja katika kuhakikisha elimu ya watu wazima inakuwa ya manufaa kwa jamii nzima kwani kutasaidia Serikali ya awamu ya Sita katika kufikia azma ya Tanzania ya viwanda ikiwa na watu wenye uelewa wa pamoja.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.