Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe.Hassan Elias Masala amefanya kikao kazi na watendaji wa kata,viongozi wa masoko na minada wa Manispaa ikiwa ni sehemu ya kupata maoni na mawazo ya namna bora zaidi ya kuhakikisha wafanyabiashara wote wa Manispaa ya Ilemela wananufaika na biashara zao wakiwa maeneo salama.
"Uwepo wa masoko na minada upo kiutaratibu,zipo sheria zinazotuongoza katika uendeshaji wake na ndio maana biashara hizi ni moja ya vyanzo vya mapato ya ndani ya Manispaa hivyo ni lazima kuweka miundo mbinu rafiki kwa wafanyabiashara wetu." Mhe.Masala
Viongozi hao wamejadili mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na suala la wafanyabiashara wote kurudi maeneo rasmi yaliyotengwa sambamba na kuendelea kuweka mipango mizuri ya uendeshaji wa minada itakayokuwa na tija kwa wote.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.