Mthamini Mkuu OR-TAMISEMI Richard Kihenga Chacha ameongoza timu ya wataalam kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI kutoa mafunzo ya uwezeshwaji kwa wataalam wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kuhusu mfumo wa ukusanyaji wa kodi za majengo ndani ya Manispaa hiyo.
"Serikali imetoa muongozo wa ukusanyaji wa kodi ya majengo,kodi ya pango la ardhi na ushuru wa mabango kwa mamlaka za serikali za mitaa tupo hapa kuhakikisha hatumuachi mtu na kupitia kuelewa kwenu itakuwa rahisi wananchi kuelewa utekelezaji wa zoezi zima ambalo litazingatia sheria za nchi,kanuni,miongozo na nyaraka mbalimbali za kiserikali kuhusu ukusanyaji wa mapato."Amesema Chacha
Akiwasilisha mada ya ukusanyaji kodi ya majengo kwa watendaji wa kata na mitaa Mthamini wa Manispaa hiyo ndugu Julius Masunga amewataka watendaji kuunga mkono juhudi za serikali katika kufanikisha zoezi hilo.
" Tunatambua nafasi ya watendaji wa kata na mitaa katika maeneo mliyopo kwa ukaribu uliopo na wananchi hivyo ni jukumu letu kuendelea kuelimisha jamii kuhusu kodi hii ya majengo ambayo Halmashauri inawajibika katika zoezi la ukusanyaji wake." Amesema Masunga
Akitoa maelekezo ya namna mfumo utakavyofanya kazi kupitia simu janja za mkononi Afisa TEHAMA wa Manispaa hiyo Albert Kamuhabwa amesema ni muhimu majengo yote kutambuliwa kurahisisha zoezi la ukusanyaji wa mapato ya kodi ya majengo.
Albert Arevoy ni Mtendaji wa kata mtaa wa Chabakima kata ya Shibula yeye anapongeza serikali kwa kuanzia mifumo mbalimbali ya ukusanyaji wa mapato kwani ni njia salama katika kudhibiti mianya ya upotevu wa mapato.
Manispaa ya Ilemela inaendelea na matumizi ya mifumo mbalimbali ya kiserikali katika utendaji kazi wake ikiwemo E - board mfumo wa uendeshaji vikao,E - office mfumo wa ufuatiliaji mafaili,Got homis mfumo unaotumika kwenye vituo vya kutolea huduma za afya n.k.ikiwa ni katika kuongeza uwazi,uwajibikaji na ufanisi .
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.