Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa kushirikiana na jiji la Daegu la nchini Korea Kusini zimetiliana saini hati ya makubaliano ya ushirikiano (MoU) wa mradi wa kusimamia na kudhibiti majanga mbalimbali kama vile ya moto, mafuriko na mengineyo, mradi unaotarajiwa kugharimu zaidi ya Dola milioni tano za kimarekani.
Zoezi hilo la utiaji saini wa makubaliano hayo lilishuhudiwa na Mkuu wa Wilaya ya Ilemela,Mstahiki Meya , Kaimu Mkurugenzi, wataalam mbalimbali wa Ilemela, vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na viongozi mbalimbali lilitanguliwa na uwasilishaji wa taarifa ya upembuzi yakinifu ya kudhibiti majanga katika maeneo yaliyopo katika Wilaya ya Ilemela.
Akizungumza katika hafla hiyo, kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela Ndugu Daniel Batare, aliishukuru serikali ya Korea kwa ushirikiano wanaoutoa katika kuiletea maendeleo Manispaa ya Ilemela. Aliongeza kusema kuwa anaamini kuwa mradi huu utawasaidia watu wa Ilemlea kukabiliana na majanga lakini pia mfumo huu utarahisisha na kuharakisha mawasiliano.
Nae Dkt. Hag II Kim ambae ni kiongozi wa timu iliyofika Ilemela, alisema kuwa mradi huu utasaidia kuokoa fedha ambazo zingepotea kutokana na kuhudumia waathirika wa majanga na badala yake zitapelekwa kwenye huduma zingine.Aliwashukuru pia ilemela kwa ushirikiano waliotoa katika kufanikisha maandalizi ya mradi huu.
Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe.Dkt Severine Lalika akihitimisha zoezi hili la utiaji saini alishukuru na kusem kuwa, anathamini sana juhudi zinazoonyeshwa na wakorea kwa ajili ya Maendeleo ya wana Ilemela huku akiwahakikishia kuendeleza ushirikiano huu ulioanza toka mwaka 2016.
Mradi huu ni matunda ya jitihada za Mhe Mbunge wa Ilemela Angeline Mabula ambae ndie muasisi wa ushirikiano na urafiki kati ya jiji la Daegu na Manispaa ya Ilemelakatika shughuli mbalimbali za kijamii lengo ikiwa ni kuboresha maisha ya wana Ilemela.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.