Na Paschalia George, Afisa Habari Ilemela
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela imeendelea kutambua vipaji vya watoto wenye ulemavu kupitia ushiriki wao katika michezo maalum inayowahusu watoto hao.
Hayo yamebainishwa na Benatus Kahuru afisa elimu maalum ambae alimwakilisha Afisa Elimu Msingi wa Ilemela katika mashindano yanayoendelea ya kuwania kombe la michezo Maalum
“Wapo watoto walemavu ambao wanafanya vitu vikubwa vya kustaajabisha ambavyo wakati mwingine hata wasio na ulemavu hawawezi kufanya,tutaendelea kuwa karibu na walimu wao ambao wanashinda nao kila siku na kuwatambua vizuri. Tunawapongeza walimu wa watoto hawa kwani wao ndio wamefanikisha kupatikana kwa wachezaji hawa ngazi ya shule, wilaya na mpaka sasa tunaelekea ngazi ya mkoa’’ alisema Kahuru
Mechi za mchujo za mashindano ya kombe la michezo maalum kwa watoto wenye ulemavu wilayani Ilemela zinaendelea kurindima ambapo wachezaji kutoka shule kumi za watoto wenye ulemavu na usonji ndani ya manispaa ya Ilemela wanatarajia kuunda timu moja itakayoshiriki mashindano hayo kimkoa.
Nae mwenyekiti wa shirikisho la walimu ambao ni makada wa CCM mkoa wa Mwanza akiambatana na baadhi ya wajumbe walikabidhi zawadi mbalimbali kwa washiriki ikiwa ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za manispaa ya Ilemela katika kuwapa nafasi watoto walemavu kucheza na kuwatia moyo na wao wajione ni kama watoto wengine.
“Tunatoa pongezi kwa uongozi wote wa Ilemela kwa kutangaza na kutambua vipaji vilivyomo katika shule zenu kumi zinazotoa elimu maalum kwa watoto wenye ulemavu mbalimbali,tuko pamoja kwa hiki tulichotoa hapa leo kikawafae watoto wetu kama burudani na kwa hatua za ukuaji wao’’Alisema Mwenyekiti.
Tumaini Richard ni mwanafunzi mwenye ulemavu wa kusikia kutoka shule ya msingi Ibeshi ametoa shukrani kwa wote walioandaa mashindano na kuwaletea vyakula na wao kupata nafasi ya kujumuika na wenzao kutoka shule za jirani na kuimarisha viungo vyao kupitia michezo mbalimbali iliyochezwa.
Michezo iliyochezwa ni pamoja na riadha iliyohusisha watoto wenye tatizo la ubongo ‘’cerebral parlsy” ,mpira wa miguu ,mpira wa kikapu na mpira wa wavu. Ambapo kwa mpira wa miguu mechi zilizoshiriki ni kanda ya Buswelu na Kanda ya Ibeshi ambao wametoka 4-0 huku mabao matatu ya kanda ya Buswelu yakifungwa na Dickson Mussa kutoka shule ya msingi Buswelu sambamba na kanda ya Kirumba na kanda ya Pasiansi ambao wametoka 1-1 hivyo washindi waliopatikana hapo katika kila mchezo wataunda timu moja itakayoshiriki mashindano hayo kimkoa
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.