Katika mwaka wa fedha 2019/20 Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela inakadiria kukusanya jumla ya Tsh.8,878,387,000. 00 kutoka vyanzo vya ndani. Sababu zilizopelekea kufikia makisio haya ni pamoja na takwimu halisi zilizokusanywa kutoka vyanzo mbalimbali, mwenenendo wa ukusanyaji mapato kutoka vyanzo mbalimbali kwa miaka ya nyuma, mabadiliko ya sheria mbalimbali yanayohusu tozo na kodi mbalimbali.
Chanzo hicho cha ndani, kinafanya jumla kuu ya makisio ya bajeti ya mapato kutoka katika vyanzo vya ndani na serikali kuu kwa mwaka wa fedha 2019/2020 kuwa kiasi cha Shilingi 75,891,541,247.98 za kitanzania, ambapo ruzuku ya miradi ya maendeleo imekisiwa kuwa kiasi cha Shilingi 23,453,644,376.00,ruzuku ya matumizi ya kawaida ikiwa Shilingi 2,011,687,870.98, mishahara Shilingi 41,547,622,000.00 na mapato ya ndani shilingi 8,878,487,000.00
Makadirio ya bajeti hii kwa mwaka wa fedha 2019/2020 yamelenga katika matumizi ya kawaida pamoja na matumizi ya miradi mbalimbali ya maendeleo. Aidha maeneo ya vipaumbele kwa bajeti hiyo yameainishwa kuwa ni pamoja na sekta ya ujenzi ,afya,utawala,elimu sekondari na msingi, Maendeleo ya jamii, ardhi na mmipangomiji maji, uvuvi na mifugo, usafishaji na mazingira, kilimo pamoja na misitu na nyuki.
Kwa upande wa ujenzi shughuli zitakazotekelezwa ni ujenzi na ukarabati wa barabara kwa kiwango cha lami na changarawe,kwa upande wa sekta ya afya shughuli zitakazotekelezwa ni ukamilishaji wa ujenzi wa hospitali ya wilaya, utoaji wa huduma za lishe na uboreshaji wa huduma za afya katika vituo vya afya 3 na zahanati 13.
Aidha shughuli zitakazotekelezwa katika sekta ya utawala ni ujenzi wa jengo la utawala, pamoja na uboreshaji wa majengo yalipo kwenye katika halmashauri ikiwemo ofisi za kata.Elimu Msini na Elimu sekondari shughuli zitakazotekelezwa ni ujenzi wa bweni katika shule ya sekondari sangabye, ujenzi wa ofisi na nyumba za walimu na vyumba vya madarasa pamoja na uboreshaji wa miunombinu ya shule.
Katika sekta ya maendeleo ya jamii fedha zitaelekezwa katika miradi ya kudhibiti UKIMWI na uwezeshaji wa vikundi vya wanawake, vijana na walemavu. Sekta ya ardhi na mipangomiji itatekeleza shughuli za uthamini, upimaji wa viwanja ikiwa ni pamoja na ulipaji wa fidia na uendelezaji wa eneo maalum la ukanda wa kiuchumi.
Shughuli zitakaotekelezwa katika sekta maji ni pamoja na kuongeza upatikanaji wa maji safi na salamakatika maeneo ya pembezoni kwa kuwezesha ujenzi wa miundombinu ya maji.Pamoja na hayo sekta ya uvuvi imejipanga kutekeleza shughuli za ukarabati na umaliziaji wa miundombinu katika machinjio ndogo za Igombe na Kayenze, uboreshaji wa mialo yote pamoja na ujenzi w daraja la kupandia na kushukia abiria kwatika mwalo wa Kirumba.
Halikadhalika sekta ya usafishaji na mazingira imejipanga kuimarisha usafi na mazingira kwa kuondoa taka ngumu kwa kushirikisha jamii.Kwa upande wa kilimo sekta imejipanga kujena jengo la kusindika unga wa mhogo katika kata ya Kayenze pamoja na kutoa mafunzo na kukabiliana na majanga mbalimbali.Katika sekta ya Nyuki/Misitu ilemela itahakikisha inatoa elimu ya mazingira, kuotesha miche ya miti pamoja na kutengeneza mizinga ya nyuki na kuigawa kwenye vikundi.
Zipo changamoto mbalimbali ambazo halmashauri imekuwa ikikabiliana nazo katika katika kutekeleza majukumu yake ni pamoja na uwezo mdogo wa Halmashauri katika kutoa huduma za kijamii hasa katika sekta ya Elimu, Afya, Maji na Miundombinu kutokana na ufinyu wa Bajeti ikilinganishwa na mahitaji,.
Hivyo katika kukabiliana na changamoto zilizopo katika Halmashauri, mikakati ya kuongeza mapato ya vyanzo vya ndani imewekwa ili kuhakikisha kuwa mapato yanakusanywa kwa ufanisi ili kufikia malengo ya kutekeleza shughuli mbalimbali kwa kuongeza uwezo wa halmashauri kujitegemea.
Baadhi ya mikakati ni pamoja na, kuongeza nguvu katika ufuatiliaji wa mapato na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara, kupitia Sheria ndogo za Halmashauri za mapato ili kufanya marekebisho ya viwango vya ushuru na kodi, Kuendelea kutoa elimu kwa mawakala na walipa kodi kuendelea kuimarisha mfumo wa utunzaji takwimu na kumbukumbu za walipa kodi, Kuchukua hatua zaidi za kisheria kwa wanaoshindwa kulipa ada na tozo mbalimbali za Halmashauri, Kuongeza idadi ya mashine za kielektroniki za kukusanyia mapato katika vyanzo vyote, Maandalizi ya mradi wa kimkakati wa “Nyamhongolo Bus and Truck Terminal, Maandalizi ya Mpango Kabambe wa eneo la uwekezaji (industrial Park) eneo la Nyamhongolo uko kwenye hatua za mwisho za kukamilika. Kushirikiana na Wahisani (World Bank, UNCDF) katika uboreshaji wa ujenzi wa miundo mbinu ya vyanzo vya mapato kama vile Masoko, Jengo la Machinga na Nyumba za Makazi.
Kwa mwaka huu wa fedha 2018/19 ,Ilemela ilijipanga kukusanya kiasi cha Shilingi za kitanzania 9,024,065,000.00 ambapo mapato halisi yaliyokusanywa hadi kufikia Desemba 2018, ni Shilingi 3,818,961,26.78 sawa na asilimia 42.3.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.