Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe CPA Amos Makalla amezitaka taasisi za umma kama vile MWAUWASA, LATRA, TANESCO kuhakikisha wanatoa kipaumbele katika utoaji wa huduma za msingi katika hospitali ya Wilaya ya Ilemela ili kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi
Mhe Makalla ametoa maelekezo hayo alipofika katika hospitali ya Wilaya kwa ajili ya kukagua ukamilishaji wa miundombinu ya hospitali hiyo.
Akitoa maelekezo hayo amewataka MWAUWASA kujiridhisha na uwepo wa huduma ya maji ya uhakika katika hospitali ya wilaya na kuhakikisha kuwa wanatoa kipaumbele katika hospitali hiyo ili huduma ziweze kutolewa kwa uhakika na ubora
“MWAUWASA mjiridhishe juu ya utoaji wa huduma ya maji katika hospitali hii ya Wilaya na utoaji wa maji uwe wa uhakika na hospitali hii ipewe kipaumbele, watumishi hawataweza kufanya kazi vizuri kama hakuna huduma ya maji ya uhakika”, alisisitiza Mhe Makalla
Sambamba na maelekezo hayo kwa MWAUWASA, ameitaka LATRA, Afisa usafirshaji Mkoa na Wilaya kuhakikisha magari yanafika hospitali ya Wilaya ili kuwarahisishia wananchi usafiri wa kufika hospitali ili waweze kupata huduma na kumtaka Mkuu wa Wilaya kusimamia utekelezaji wa agizo hilo.
“Nimetoka kukagua ujenzi wa barabara na nimeona jiografia ya huku, naamini itarahisiha wananchi kuja huku, maelekezo yangu ni kwa LATRA, Afisa usafirishaji Mkoa na Wilaya kuweka utaratibu wa magari yanayotakiwa kufika huku ili kuwarahisishia wananchi kufika hospitali ya wilaya na kupata huduma”
Mhe Makalla alitumia nafasi hiyo kuwapongeza watumishi wa idara ya afya kwa kazi kubwa wanayofanya ya kuhudumia wananchi huku akiwasihi kusimamia na kuitimiza dhamira ya Rais ya kutoa huduma bora kwa wananchi.
Akisoma taarifa Mganga Mkuu wa Manispaa ya Ilemela, Dr. Samson Marwa amesema kuwa kwa sasa Hospitali hiyo ya Wilaya inatoa huduma kwa wagonjwa wa nje tuu (OPD) ambapo tangu ianze kutoa huduma mwaka 2020 hadi 2023 imeshahudumia jumla ya wagonjwa 7079 na akaongeza kusema kuwa itakapokamilika kwa asilimia 100 itarahisisha upatikanaji wa huduma za afya kwa wananchi wa maeneo ya Wilaya ya Ilemela na maeneo jirani.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.