Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela inatekeleza Mpango wa Maendeleo wa Sekta ya Maji (WSDP) kupitia Mpango wa Kitaifa wa Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (NRWSSP), katika maeneo ya pembezoni yenye sura ya vijiji, ambapo kati kata 19 za Manispaa ni kata 4 ndizo zina sura ya vijiji ambazo ni Kayenze, Sangabuye, Shibula, Bugogwa na sehemu ya kata ya Kahama.
Kupitia program utekelezaji wa miradi ya maji ya vijiji 10 katika maeneo ya Kayenze, Sangabuye, Igombe, Nyafula Igogwe, Kabusungu, Nyamwilolelwa, Kahama na Nyamadoke ipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.
Mradi wa maji wa Igombe ni moja ya mradi ambao unatekelezwa kupitia mradi wa maji ya vijiji 10.
Kwa sasa mradi huu upo katika hatua za ukamilishaji ambapo zoezi lililopo ni la ulazaji wa bomba linalotoa maji ziwani kuelekea katika pampu ya maji.
Mradi huu unatarajiwa kutoa huduma ya maji safi na salama kwa wakazi wapatao 41,673 wa kata za Sangabuye, Bugogwa, Shibula, Kahama na Nyamhongolo. Hii itapelekea zaidi ya 65% ya wakazi wanaoishi maeneo yenye sura ya vijiji kupata maji safi na salama
Hadi kukamilika utakuwa umegharimu kiasi cha Shilingi, 2,158,024,000.00 ambayo ni fedha kutoka serikali kuu.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.