HALMASHAURI ZATAKIWA KUVIPA KIPAUMBELE VIKUNDI VYA KINA MAMA Halmashauri za mkoa wa Mwanza zimetakiwa kuvipa kipaumbele vikundi vyote vya kina mama katika utoaji wa Mikopo na Umiliki wa Ardhi lengo likiwa ni kuhakikisha wanawake wanajikwamua kiuchumi na kuacha utegemezi katika kujiletea maendeleo Hayo yamesemwa leo na Mbunge wa Jimbo la Ilemela na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi alipokuwa akizungumza na Wanawake wa Mkoa wa Mwanza katika kilele cha maadhimisho ya sherehe za siku ya Wanawake Duniani ikiwa na Kauli Mbiu kuwa Tanzania ya Viwanda Wanawake ni Msingi wa Mabadiliko Kiuchumi ambapo kimkoa yamefanyika Viwanja vya Furahisha wilayani Ilemela. Akizungumza katika maadhimisho hayo Mheshimiwa Mabula amewataka Wanawake kuzitumia fursa za umiliki wa Ardhi ili kuongeza uzalishaji wa bidhaa zao sambamba na kuwataka viongozi wanawake wa maeneo hayo kusimamia upatikanaji wa stahiki za wanawake huku akizitaka kushirikiana na asasi zisizo za kiserikali katika kutoa elimu na kuwapata washauri wa msaada wa kisheria … Kama Serikali tunapenda kuwaona watu mnafanya shughuli katika mazingira mazuri ambayo yanatambulika na ni rahisi pia kupata huduma kutoka Serikalini kwa vyovyote vile ukiwa kwenye eneo linalotambulika utahudumiwa na utatambulika lakini ukiwa kwenye eneo ambalo halitambuliki itakuwa kazi pia hata wewe kutambulika …’ Aidha amevitaka vikundi vya walemavu kuacha kujiona wapweke na kuzitumia fursa zilizopo katika kujikwamua Akisoma risala kwa Mgeni rasmi kwa niaba ya wanawake Ndugu Mary Muhoha amelalamikia kuwepo kwa vitendo vya Ukatili, Uonevu na Unyanyasaji na kuitaka Jamii na Serikali kuungana kuondoa changamoto hizo hizo Akihitimisha kwa niaba ya Wanawake wote waliojitokeza viwanjani hapo Mbunge wa Viti maalum Mkoa wa Mwanza Mheshimiwa Kiteto Zawadi Koshuma mbali na kumshukuru Mgeni rasmi kwa kujitoa kwake na kushiriki pamoja katika kuadhimisha sherehe hizo na amemuomba tena kuwa Mgeni rasmi katika sherehe ya ufunguzi wa kiwanda cha kwanza kitachomilikiwa na Wanawake wa Mkoa Mwanza bila kujali tofauti zao kitachojihusisha na Usindikaji wa Viungo na Karanga mapema mwakani.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.