Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini A Unguja yafanya ziara katika Manispaa ya Ilemela kwa lengo la kujifunza suala zima la Ukusanyaji wa mapato pamoja na namna ambavyo Ilemela inasimamia utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Wakiwa Ilemela walipatiwa taarifa mbalibali za miradi pamoja na kuelezwa namna ambavyo Ilemela imejipanga katika suala zima la ukusanyaji wa mapato.
Pia walipata fursa ya kutembelea miradi ikiwemo mradi wa ujenzi wa jengo la utawala,ujenzi wa barabara ya Sabasaba-Kiseke-Buswelu, Ujenzi wa mzani wa kupimia mazao ya samaki katika soko la kimataifa la samaki lililopo Kirumba, ujenzi wa madarasa katika shule ya sekondari Buswelu.
Aidha wakiwa katika ziara hiyo walipata fursa ya kuuliza maswali mbalimbali nakupatiwa majibu na kubwa zaidi ikiwa ni namna gani ilemela inasimamia ukusanyaji wa mapato katika vyanzo mbalimbali.
Katika kuhitimisha wageni hao waliipongeza timu nzima ya Ilemela kwa namna ambavyo inashirikiana katika kuhakikisha utekelezaji wa miradi mbalimbali pamoja na uusanyaji wa mapato unafanikiwa.Pia waishukuru kwa ushirikiano uliotolewa na wataalam wa Manispaa katika ziara hiyo ya mafunzo.
Ziara hii iliongozwa na Katibu Tawala Mkoa wa Unguja, ikijuuisha waheshimiwa madiwani pamoja na wataalam kutoka Halmashauri ya Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.