Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe. Dkt. Angeline Mabula amewatoa hofu wananchi wa kata ya Shibula kuwa hakuna mwananchi mwenye uhalali wa kulipwa fidia ya eneo lake litakaloathirika kutokana na ujenzi wa barabara mpya yenye urefu wa kilomita 46 kutoka uwanja wa ndege uliopo Manispaa ya Ilemela kuelekea Nyanguge wilayani Magu bila kulipwa haki yake.
Ameyasema hayo wakati wa mkutano wake wa hadhara wa kusikiliza kero za wananchi katika viwanja vya Mhonze kata ya Shibula ambapo amesema kuwa Serikali imekwisha tenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo ambayo ilikuwa kero kwa muda mrefu kwa wananchi wa eneo hilo .
“.. Tulikuwa na kero ya muda mrefu ya ukosefu wa barabara sasa serikali ya Dkt. Samia imetuletea fedha tujenge, mlitaka maendeleo serikali imesikia kilio chenu,niwahakikishie hakuna mwenye haki atakaekosa stahiki yake ..” Alisema
Aidha Mhe Dkt Mabula amewaasa wananchi hao kushiriki katika shughuli za maendeleo pamoja na kujitokeza katika kujiandikisha kwenye daftari la uchaguzi wa serikali za mtaa kwa mwaka 2024 na kujitokeza kwa wingi Oktoba 03 kilele cha mbio za Mwenge wa uhuru mkoani Mwanza viwanja vya CCM Kirumba.
Kwa upande wake mkuu wa idara ya mipango kutoka wakala wa barabara mkoani Mwanza TANROADS Mhandisi Magesa Mwita amesema kuwa upembuzi yakinifu wa barabara ya kutoka uwanja wa ndege kuelekea Nyanguge ulifanywa na mzabuni na baadae wao kama taasisi waliurudia upya ili kuondoa malalamiko yaliyoibuka na kuwahakikishia kuwa hakuna uonevu wowote uliofanyika na kama kutakuwa na malalamiko mengine wapo tayari kukaa meza moja na walalamikaji kwa ajili ya suluhu huku akisisitiza kuwa wamefuata sheria na taratibu za ujenzi huo na kuwa kila mwananchi mwenye haki ya kulipwa atalipwa kabla ya nyumba zake kuvunjwa .
Mhe. Renatus Babehe Mulunga ni mstahiki meya wa manispaa ya Ilemela mbali na kuishukuru serikali ya Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo ndani ya manispaa yake, amewataka wananchi wa kata hiyo kuendelea kushirikiana na serikali kupitia sera ya manispaa hiyo ya utatu
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.