Katika kuhakikisha kuwa mtoto wa kike anasoma vizuri akiwa katika mazingira rafiki, Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kupitia fedha za EPFR imeweza kukamilisha ujenzi wa bweni la wasichana katika shule ya Sekondari ya Buswelu.
Bweni hili lenye jumla ya vyumba vya kulala 20, vyoo, bafu na sehemu ya kufulia ambalo linatarajiwa kuchukua wanafunzi 80 kwa mara moja limegharimu kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 102,962,000 ikiwa milioni themanini ni fedha za EP4R, Shilingi milioni 21,962,000 ni fedha za mapato ya ndani za Halmashauri na shilingi milioni moja ni fedha za wananchi.
Kutolewa kwa fedha hizo za EPFR kutoka serikali kuu ni kutokana na Halmashauri kufanya vizuri kitaaluma kwa mwaka wa fedha 2020/2021 kwa kiwango cha kukidhi vigezo kupata fedha hizo.
Mwl. Peter Arsen ambae ni Mkuu wa Shule ya Sekondari Buswelu, amezitaja faida za kukamilika kwa bweni hilo kwa mabinti wa kidato cha tano na sita ambao ndio wanufaika wakuu wa mradi huo na kusema kuwa itaongeza idadi ya wanafunzi wa bweni ambao watajiunga na kidato cha tano na sita ambapo itaongeza tahasusi zingine za sayansi, sambamba na kukomesha tatizo la ujauzito mashuleni.
Aliendelea kusema kuwa kwa hivi sasa shule ya sekondari Buswelu imekuwa na mazingira mazuri ya kuvutia katika kujifunzia na kufundishia kama anavyobainisha mwalimu mkuu wake Mwl. Arsen Peter
“Kukamilika kwa bweni hilo ni manufaa makubwa kwa mabinti zetu wa kidato cha tano na sita ambao watakuwa wakipata elimu katika mazingira rafiki na ya uhakika wa kufanya vizuri katika masomo yao” amesema Mwl.Peter
Placidia Mbatina na stela stephano ambao wote ni wanafunzi wa kidato cha sita wa mchepuo wa PCB katika shule ya sekondari Buswelu, wamesema kuwa kujengwa kwa bweni hili kutasaidia kuongeza ufaulu mzuri katika mitihani mbalimbali ya ndani nay a kitaifa huku wakiishukuru serikali na kuahidi kuwa watahakikisha wanafanya vizuri katika masomo yao.
“Tunajivunia kusoma shule yenye mazingira mazuri kama haya,ni faida kwetu kwani kutaongeza ufaulu na kuepusha vishawishi mbalimbali vya mtaani kwa sisi mabinti tulio na malengo ya kufika mbali kielimu”
Shule ya sekondari Buswelu ni miongoni mwa shule 27 za serikali iliyopo ndani ya kata ya Buswelu katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.