Kila mwaka tarehe 16 Juni, Tanzania inaungana na nchi zingine za Afrika kuadhimisha siku ya mtoto wa Afrika .
Chimbuko la maadhimisho hayo lilitokana na makubaliano ya umoja wa nchi huru za Afrika (kipindi hicho O.A.U) mnamo mwaka 1990 kwa lengo la kuwakumbuka watoto wa Soweto nchini Afrika kusini waliouawa kikatili kwa kupigwa risasi wakiwa katika maandamano ya amani kudai haki zao za msingi Juni 16 ,1976.
Zaidi ya watoto 176 waliuawa wakati wakidai haki ya kutobaguliwa pamoja na kupata elimu bora na kupinga mifumo ya elimu ya kibaguzi iliyokuwepo wakati huo chini ya utawala wa ubaguzi wa rangi wa kikaburu.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kwa kushirikiana na wadau imeadhimisha siku hii kwa kutoa elimu kwa jamii juu haki na ulinzi wa mtoto,elimu ya kujitambua, kutambua haki na wajibu kwa watoto wenyewe sambamba na michezo mbalimbali kuwakumbusha michezo ni Afya na furaha.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.