Walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) wametakiwa kuimarisha vikundi vyao kwa kubuni shughuli mbalimbali za uzalishaji ambazo zitaweza kuwaletea unafuu wa maisha.
Wito huo umetolewa na Bi Deograsia Lubuga ambae alimuwakilisha mratibu wa TASAF wakati walengwa hao wakipatiwa elimu juu ya matumizi ya fedha zitakazotolewa.
Aidha amewataka wanufaika wa mpango huu kutumia pesa zao kwa utaratibu mzuri wa kuwaletea manufaa na kutahadharisha kuwa lengo la mradi ni kunusuru kaya maskini hivyo jamii bado ina wahitaji wengi, wale waliopata nafasi ya kuwa walengwa wasilemae katika kufanya chochote kitakachowainua kiuchumi.
“Huu ni mradi wa kunusuru kaya maskini ambao huwa tunafanya kwa kipindi cha miaka mitatu mitatu,wahitaji ni wengi mno ndani ya jamii yetu,nyinyi ambao tayari ni walengwa wa mradi mnapaswa kutumia kipindi chenu vizuri kwa kujiwekeza kidogokidogo kwa kadri mnavyopata angalau kuhakikisha una kitu cha kukusogeza kimaisha.” Amesema Bi.Deograsia
Elimu mbalimbali zimetolewa ikiwemo kuhusiana na ajira za muda na uendelezaji wa miundo mbinu imetolewa pia kwani lengo la miradi hii ni kuongeza kipato na ujuzi kwa walengwa wanaojiweza kwa maana ya kuwa na uwezo wa kufanya kazi mbalimbali za kuendeleza miundo mbinu ya jamii kama vile barabara ,madarasa na hifadhi ya mazingira.
Esta Malucha Shigela ni mmoja wa wanufaika wa mpango wa kunusuru kaya maskini Ilemela katika mtaa wa Bujingwa ndani ya kata ya Buswelu anasema toka aingie kwenye mpango anaona utofauti wa maisha aliyokuwa nayo awali na sasa hivyo ameishukuru serikali kwa kuwawezesha wahitaji.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela inaendelea na zoezi la uhawilishaji fedha kwa walengwa wa mpango wa kunusuru kaya maskini (TASAF) kwa kipindi cha Septemba-Octoba 2022 ambapo jumla ya shilingi za kitanzania 302. 89 zinatarajiwa kutolewa kwa kaya 5843 zinazopatikana ndani ya kata 19 za Manispaa ya Ilemela.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.