Katika majengo ya hospitali ya Wilaya niliyopitia na kukagua, ninaipa Alama A hospitali ya wilaya ya Ilemela, Alisema Naibu Katibu Mkuu wa OR-TAMISEMI Dkt.Dorothy Gwajima.
Kauli hiyo aliitoa alipokuwa katika ziara ya kikazi katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ambayo ilikuwa na lengo la kuangalia shughuli za utekelezaji wa afya katika mikoa na halmashauri, ikiwa ni pamoja na kuangalia miradi ya maendeleo imefikia wapi ambayo ni ujenzi wa vituo vya kutolea huduma za Afya na hospitali za Halmashauri za Wilaya mpya zilizopewa pesa Bilioni 1.5 kutoka serikali kuu.
Pamoja na hayo ziara hii ililenga pia kuangalia ni namna gani wataalam wa afya wamejiandaaje kutoa huduma katika hospitali hii mpya ya wilaya, kuangalia utayari wao wa kutoa huduma bora kwani malalamiko ya wananchi katika kupokea huduma yamekuwa mengi hivyo tunataka watumishi walioandaliwa.
“Tusiishie kuwa na majengo mazuri tu bali tuwe na mifumo laini (watumishi bora) ili wananchi wafurahi huduma”,alisisitiza Gwajima
Aliongeza kwa kusema kuwa mifumo laini haiwezi kusimama kwa kuwa na watu wanaobebwa, itasimama kwa watu watakaojisimamia wao wenyewe bila mbeleko na kwa takwimu.
Aidha alimshukuru na kumpongeza Mkurugenzi kwa utayari wake wa kutumia fedha za mapato ya ndani kwa ajili ya kuhakikisha kuwa Hospitali inakamilika.
“Hospitali imejengwa vizuri kwa viwango yaani thamani ya pesa imeonekana, na ile pesa iliyopelea ninamshukuru Mkurugenzi wa Manispaa kwa sababu yupo katika kutumia vyanzo za ndani ili kuendelea kuikamilisha”.
Mwisho, amewataka viongozi ambao wako kwenye mradi huo wa hospitali kuendelea kufanya kazi kwa ushirikiano ili yale yaliyobakia yaweze kukamilika, na kuwaagiza viongozi kuhakikisha kuwa utekelezaji ufanyike kwa yale aliyoyarekebisha kwenye baaadhi ya majengo ya Hospitali hiyo ili ifikapo mwezi wa kwanza 2020 huduma zianze kutolewa .
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.