Wananchi wa wilaya ya Ilemela wana kila sababu ya kumpongeza na kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hasan kwa kutoa fedha za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kipindi cha mwaka mmoja tangu aingie madarakani.
Akizungumzia mafanikio ya siku 365 za Rais Samia tangu kuingia madarakani katika ukumbi wa Malaika Beach Resort Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Mwalimu Hasan Elias Masala amesema kuwa kwa kipindi cha mwaka mmoja ndani ya wilaya yake Mhe Rais ametoa kiasi cha shilingi bilioni tatu na nusu kwaajili ya zoezi la upimaji, upangaji, umilikishaji na urasimishaji wa makazi, shilingi milioni mia na hamsini kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati tatu, shilingi bilioni moja na milioni mia tisa na nne kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, milioni mia tano kwa ajili ya ujenzi wa kituo kipya cha afya Kayenze na milioni mia nne na sabini kwa ajili ya ujenzi wa sekondari ya kata ya Buzuruga.
‘.. Ndugu zangu hatuna cha kusema zaidi ya kumuombea kwa Mungu na kumshukuru, Sisi wana Ilemela tunapaswa kusema Ahsante Mhe Rais kwa fedha nyingi za maendeleo na tunaahidi kuzisimamia ...’ Alisema
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ilemela ambae pia ni Waziri wa Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe Dkt Angeline Mabula amesema kuwa kwa nchi nzima Mhe Rais Samia Suluhu Hasan kupitia wizara anayoisimamia ametoa kiasi cha shilingi bilioni hamsini kwaajili ya upangaji, upimaji na urasimishaji wa makazi fedha ambazo zitasaidia kupunguza migogoro ya ardhi kwa kuwa maeneo mengi yatakuwa yamepimwa ikiwemo Ilemela huku akishukuru kwa fedha nyengine zilizotolewa hivi karibuni kiasi cha dola milioni 150 sawa na shilingi bilioni 345 kwaajili ya kuimarisha mifumo ya Tehama, uimarishaji wa ofisi na upimaji.
Nae Mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela Mhandisi Modest Joseph Apolinary amesema kuwa manispaa yake imeanza kujikita katika kutegemea uchumi wa bluu kupitia ziwa viktoria ambapo fedha zimetengwa kwa ajili ya maboresho ya mialo inayopatikana ndani ya wilaya hiyo ili kuongeza mapato na kuwakwamua wananchi kiuchumi.
Modest John ni mwenyekiti wa chama cha wafanya biashara wadogo wadogo maarufu machinga kwa wilaya ya Ilemela ambapo ameishukuru Serikali ya Rais Samia kwa kuwajali wafanya biashara hao kwa kutoa fedha za uboreshaji wa masoko, mitaji na upangaji katika maeneo rasmi ya biashara ndani ya siku 365 za uongozi wake.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.