Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hasan ni kinara na mfano wa kuigwa katika kutunza, kuhifadhi na kulinda mazingira nchini .
Hayo yamesemwa na Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mwl.Hasan Elias Masala wakati wa hafla ya kukabidhi mitungi ya gesi kama nishati rafiki kwa mazingira iliyotolewa na Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe. Dkt Angeline Mabula kwa makundi mbalimbali katika jamii wakiwemo wasanii, vijana, mabalozi wa CCM, vikundi vya mbio na wajasiriamali huku akiwataka kumuunga mkono na kumshukuru kwa utekelezaji wa miradi ya maendeleo ndani ya Ilemela.
'.. Hiki anachokifanya Mbunge wetu hii leo ni muendelezo wa juhudi za Rais wetu katika jitihada za utunzaji wa mazingira, Twendeni tukaitumie vizuri mitungi ya gesi tuliyopewa ..' Alisema
Aidha Mhe.Masala ameongeza kuwa Rais Dkt Samia Suluhu Hasan amekuwa kielelezo katika kila sekta ya maendeleo ambapo ametoa fedha nyingi kwa ajili ya shughuli za maendeleo na wilaya ya Ilemela ni miongoni mwa wanufaika .
Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe. Dkt. Angeline Mabula mbali na kumshukuru Rais Dkt Samia Suluhu Hasan kwa utunzaji wa mazingira amewataka wananchi wa Jimbo hilo kuhakikisha wanatumia nishati safi na salama kutunza mazingira pamoja na wajasiriamali kutumia mitungi hiyo kama sehemu ya mtaji katika biashara zao na kujikwamua kiuchumi huku akiwasisitiza kuwapuuza wanaobeza na kupotosha jitihada hizo za utunzaji wa mazingira .
Bi.Ummy Mohamed Wayayu ni Mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela yeye amempongeza Mbunge Dkt. Angeline Mabula kwa juhudi zake za kuwakwamua wananchi kiuchumi sambamba na uhamasishaji wa utunzaji wa mazingira kwa kutumia nishati mbadala ya gesi.
Nae meneja wa miradi kutoka kampuni ya ORYX Ndugu Peter Ndomba amewaasa wananchi walionufaika na mitungi hiyo ya gesi kuhakikisha wanazingatia usalama na matumizi sahihi ili kujikinga na madhara yanayoweza kujitokeza ikiwemo kulipukiwa kama mitungi haitafungwa vizuri au kuwasha bila kuzingatia taratibu huku akimpongeza Mbunge Dkt Mabula kwa kazi nzuri anayoendelea nayo ya kuchochea maendeleo Ilemela.
Jumla ya mitungi mia tano kutoka kampuni ya ORYX imetolewa na Mb.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.