Mkuu wa Wilaya ya Ilemela Mhe.Hassan E.Masala amezindua rasmi huduma za afya kuanza kutolewa katika zahanati mpya ya Mihama iliyopo kata ya Kitangiri ndani ya Manispaa ya Ilemela.
Akizungumza wakati wa hafla fupi ya ufunguzi wa zahanati hiyo Mhe.Masala ametoa pongezi nyingi kwa uongozi wa kata ya Kitangiri na Manispaa kwa ujumla kwa kazi nzuri ya ukamilishaji wa ujenzi wa zahanati hiyo.
"Kwenye mafanikio yoyote changamoto hazikosekani, muhimu kufanikisha jambo."
Aidha Mhe.Masala kipekee amewapongeza mabalozi 13 wa mitaa ya Mihama kwa kazi nzuri ya kuunganisha wanaMihama kwa kipindi chote cha ujenzi.
Ametoa rai kwa wahudumu wa afya katika zahanati hiyo kuhakikisha wanatoa huduma bora kwa wananchi ili lengo halisi la kuwepo kwa zahanati hiyo lionekane .
Nae diwani wa kata ya Kitangiri Mhe.Donald Ndaro amemshukuru na kumpongeza Mkuu wa Wilaya hiyo huku akitaja baadhi ya changamoto zilizopo ndani ya kata yake kama vile changamoto ya kujaa maji eneo hasa nyakati za mvua na kuahidi kushirikiana na uongozi katika kulitatua.
Rose Sabinus ni katibu wa tawi la CCM la Mihama yeye ametoa shukrani nyingi kwa mbunge wa Jimbo la Ilemela Mhe.Dkt.Angeline Mabula kwa kutoa msukumo mara kwa mara na kufanikisha ujenzi huo.
"Shukrani kwa serikali ya awamu ya sita kwa kutuletea zahanati hii kwani ilikuwa ni hitaji la muda mrefu,jambo hili limeondoa kero ya kusafiri umbali mrefu kama km 6 hivi kutoka hapa kwenda zahanati ya Kirumba kufuata huduma za afya."
Zahanati ya Mihama imegharimu jumla ya shilingi milioni 225 hadi kukamilika kwake ikiwa ni fedha kutoka mfuko wa mradi wa kunusuru kaya maskini (TASAF).
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.