Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mhe Dkt Mathias Severine Lalika amehimiza uwazi, uadilifu na ushirikishwaji wa wananchi katika matumizi ya fedha za ujenzi wa madarasa ya shule za sekondari zilizopo ndani ya wilaya ya Ilemela yatakayotumika na wanafunzi wanaotarajia kuanza kidato cha kwanza kwa mwaka huu 2021.
Rai hiyo ameitoa wakati wa ziara ya ukaguzi wa ujenzi wa miundombinu ya madarasa, vyoo, ofisi za walimu, viti na meza aliyoifanya akiwa pamoja na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Ilemela.
Akiwa katika ziara hiyo amewataka walimu wakuu na kamati za ujenzi kuhakikisha wanatumia vizuri fedha zilizotolewa na Serikali na michango ya wananchi kwa ajili ya kukamilisha miundombinu hiyo sanjari na kuwepo kwa ushirikishwaji na uwazi ili kuondoa minong’ono ya kutoaminiana jambo litakalodhoofisha uchangiaji wa shughuli za maendeleo kutoka kwa wananchi.
‘ Ni wajibu wa viongozi wote kuanzia ngazi za mitaa hadi wilaya kuhamasisha na kuelimisha jamii juu ya umuhimu wa kuchangia shughuli mbalimbali za kimaendeleo kama hii tuliyonayo sasa sambasamba na kutoa mirejesho chanya kwa jamii ili waone nguvu zao zinazaa matunda mazuri kwa manufaa ya watoto wetu na jamii nzima kwa ujumla’ alisema.
Alex Mkusa akimuwakilisha Afisa Elimu Sekondari, amezisisitiza kamati za ujenzi za shule husika kuhakikisha ujenzi unakamilika kwa wakati kwani Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela imeshatenga fedha zote kwa shughuli zinazoendelea na kwamba awamu ya kwanza ya fedha hizo imeshawekwa kwenye akaunti za shule zote zenye miradi ya ujenzi wa madarasa.
“Ujenzi huu ni budi ukamilike kwa wakati kwani hatuna kizuizi , mahitaji yote yapo,pesa ipo hivyo kila shule mfanye juhudi kukamilisha ujenzi wa madarasa haya kwa wakati kwani shule zetu zote zimepangiwa wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza na shule zimeshafunguliwa.Tukamilishe mradi huu kwa wakati sambamba na agizo la Waziri mkuu Mhe.Kassim Majaliwa Kassim.”alisema
Halmashauri ya Manispaa Ilemela kupitia chanzo cha mapato cha ndani kimetoa jumla ya Shilingi Milioni 252,690,000.00 tu kwa ajili ya ukamilishaji wa vyumba vya madarasa 60 kwa shule 16 za sekondari kwa awamu ya kwanza. Pamoja na hayo kupitia mradi wa matofali
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.