Uanzishwaji wa dawati la huduma za ustawi wa jamii katika vituo vya usafiri ni maelekezo ya serikali kupitia ofisi ya Rais TAMISEMI juu ya uwepo wa maafisa ustawi wa jamii katika maeneo ya bandari na stendi kuu za mabasi yaendayo mikoani tangu juni 2022
Lengo kuu la uanzishwaji wa madawati haya ni pamoja na kuimarisha utoaji wa huduma kwa makundi maalumu hususani kuzuia watoto kuingia mtaani pamoja na Kuzuia usafirishaji haramu wa binadamu (human trafficking), hasa kubaini na kuzuia watoto wanaosafirishwa kinyemela.Kusaidia watu /wananchi waliopo katika mazingira hatarishi maeneo ya stendi
"Halmashauri ya manispaa ya Ilemela ni miongoni mwa halmashauri zenye stendi kuu ya mabasi ijulikanayo kama stendi ya Nyamhongolo ambapo kupitia dawati hilo la huduma za ustawi wa jamii, ambapo katika kipindi cha machi 2024 hadi april 2025 jumla ya watoto 146 wamehudumiwa kati yao wasichana ni 81 na wavulana ni 65 na kuwa asilimia 68 ya watoto waliopatiwa huduma katika dawati hilo ni wenye umri kati ya miaka 7- 14, asilimia 31 ni watoto wenye umri wa miaka 15 -17 na asilimia moja ni watoto wenye umri wa miaka 7", Amebainisha Bi Lucy Katonkola afisa ustawi wa jamii wa manispaa ya Ilemela anaeshughulika na dawati ya huduma za ustawi wa jamii katika stendi hiyo
Sambamba na hilo bi Lucy ametoa rai kwa wazazi na walezi kuachana tabia ya kusafirisha watoto wadogo peke yao bila mtu mzima kumsimamia, pia amewataka wananchi wanaozunguka maeneo ya stendi kuhakikisha wanatoa kipaumbele katika suala la ulinzi na usalama wa watoto maeneo ya stendi
Railway Children Africa (RCA) ni shirika ambalo limekuwa likishirikiana na manispaa ya Ilemela kupitia maafisa ustawi wa jamii katika utoaji wa huduma za ustawi katika stendi hiyo ya mabasi ya Nyamhongolo.
Anitha Joseph ambae ni afisa mradi wa shirika hilo amsema kuwa wamekuwa wakijishughulisha na watoto na vijana wanaoishi katika mazingira hatarishi pamoja na familia zao huku wakilenga katika kuimarisha muitikio wa jamii juu ya watoto na vijana walio katika mazingira hatarishi hasa waliopo mitaani kwa kutoa elimu kwa jamii na namna ya kuzuia na kudhibiti wimbi la watoto hawa wa mitaani kwa kushirikiana na serikali kuzitafsiri sheria na miongozo inayolenga kuwasaidia watoto na vijana hao
Huduma za ustawi wa jamii katika stendi ya Nyamhongolo zinapatikana katika chumba namba 60 na wale wote wenye changamoto na uhitaji wa huduma za ustawi wa jamii wamehimizwa kufika katika ofisi hizo.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.