Mhe.CPA Amos Makala, Mkuu wa mkoa wa Mwanza amefika stendi ya mabasi ya Nyamhongolo kwa ajili ya kukagua na kisha kuongea na viongozi wa TABOA pamoja na wadau mbalimbali wa stendi.
Akizungumza wakati wa kikao hicho amewahimIZA watumishi wa umma kuhakikisha wanaweka mazingira bora kwa sekta binafsi ili waweze kutoa huduma bora kwa wananchi.
"Sisi tunatakiwa kuwa vinara katika kutengeneza mazingira mazuri ili sekta binafsi waweze kufanya vizuri",CPA Makalla
Aidha ameutaka uongozi wa Ilemela kushirikiana na TABOA na wadau wote ili kuweza kuiendesha vizuri stendi ya Nyamhongolo
Nae Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Adv.Kibamba Kiomoni amekiri mapungufu na kusema yupo tayari kukaa meza moja kwa ajili ya mazungumzo ili kuweka mazingira bora ya biashara
"Tupo hapa kufanya mazingira ya biashara kuwa mepesi", amesema Adv Kibamba
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.