Chama Cha Mapinduzi wilaya ya Ilemela kimefurahishwa na kuridhishwa na hatua za ujenzi wa vyumba vya madarasa yanayotokana na fedha za mpango wa maendeleo dhidi ya UVIKO-19 kiasi cha shilingi bilioni moja na milioni mia tisa na arobaini zilizotolewa hivi karibuni na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu Hassan kwa ajili ya kukamilisha vyumba 97 katika shule 26 za manispaa hiyo
Hayo yamebainishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Ilemela Ndugu Nelson Mesha wakati wa ziara ya kamati ya siasa ya chama hicho kwa ajili ya kukagua hatua za ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa ambapo amefafanua kuwa chama kimeona kazi kubwa iliyofanywa na wataalam wa manispaa hiyo kwa kushirikiana na wananchi, viongozi wa Serikali na wa chama chenyewe katika shule mbalimbali za kata za wilaya hiyo huku akisisitiza kamati za ujenzi na wataalam kuendelea na kasi hiyo ili vyumba hivyo vikamilikie kwa muda uliopangwa huku vikizingatia ubora na thamani ya fedha
‘.. Niwapongeze kwa hatua hii nzuri ya ukamilishaji wa madarasa, na bahati nzuri chama tumeshiriki pamoja kuanzia hatua za awali mpaka sasa, Mimi binafsi nimeshapita mara nyingi lakini nikaona leo tupite kwa pamoja kama wajumbe wa kamati ya siasa ili nao wajilizishe kwa kazi iliyofanyika ..’ Alisema
Aidha Mwenyekiti Mesha ameongeza kuwa Chama hicho ngazi ya wilaya kinamshukuru Rais Mhe Samia Suluhu Hassan kwa uamuzi wake wa kutoa fedha za ujenzi wa madarasa kwani hatua hiyo itasaidia kupunguza msongamano wa wanafunzi madarasani pamoja na kuwapunguzia wazazi gharama
Pamoja na pongezi hizo kamati ya siasa ya wilaya kwa ujumla wao imehimiza suala la kukamilisha madarasa hayo kwa wakati ili mwaka mpya wa elimu utakapoanza yaani 2022 watoto wote waingie darasani kama ilivyo dhamira ya Mhe. Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa meza na viti vinakuwepo.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.