Mtaalam kutoka Benki ya dunia ndugu Aquiline Safari akiambatana na wataalam kutoka wizara ya elimu sayansi na teknolojia na OR-TAMISEMI amefanya ziara ya kutembelea na kukagua utekelezaji wa miradi ya elimu ya SEQUIP katika shule za sekondari na BOOST katika shule za msingi ndani ya Manispaa ya Ilemela.
Safari amesema lengo la ziara hiyo ni kufanya tathimini ya manunuzi na matumizi ya fedha zilizotolewa sambamba na kuangalia masuala ya utawala bora kwa kuangalia ushirikishwaji wa jamii, sheria zilitumika vipi katika kipindi chote cha utekelezaji wa mradi.
"..Kazi iliyofanyika ni nzuri na thamani ya pesa inaonekana, hakuna sababu ya kumnyima pesa mtu anaetumia vizuri naamini hata zikija fedha nyingine zitatumika ipasavyo kikubwa miundo mbinu hii ilindwe ili idumu na vizazi vijavyo vikute matunda haya.."
Nae Mkurugenzi wa elimu ya awali na msingi kutoka OR-TAMISEMI Bi.Susana Nussu amesema serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imejipanga vizuri katika kujenga na kuboresha miundo mbinu mbalimbali ya elimu.
"..Elimu ndio kipaumbele chetu, tunafahamu tunalo jukumu kubwa la kuzalisha watu watakaopambana katika soko la kimataifa kielimu bila kuwa na mazingira rafiki yanayoakisi hayo itakuwa ngumu..."
Kamani Shigella ni mkazi wa mtaa wa Kabambo yeye ni mmoja wa wajumbe katika kamati ya ujenzi wa shule ya sekondari Kisenga ameomba ujenzi unaokuja uwe wa maghorofa kwa kuzingatia ufinyu wa maeneo na kuwahakikishia wataalam hao kuwa kamati ipo tayari kusimamia mradi wowote utaoletwa kwao.
Hoja ya Shigella ya ujenzi wa maghorofa imepokelewa na timu nzima ya wataalam hao huku wakiwapa nafasi wataalam wenyeji kuanza kuchakata upatikanaji wa maeneo yasiyo na migogoro na kuyapatia hati miliki.
Shule zilizotembelewa ni pamoja na Bwiru wasichana iliyopo kata ya Pasiansi, Kisenga sekondari Kiseke ilogharimu kiasi cha shilingi 584,280,000 na shule ya msingi Buteja ilokamilika kwa jumla ya kiasi cha shilingi milioni 540.3 ndani ya kata ya Kahama.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.