• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

BENKI YA DTB YAUNGANA NA ILEMELA KUMUUNGA MKONO MAKAMU WA RAIS JUU YA UTUNZAJI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA

Posted on: January 5th, 2018

BENKI YA DTB YAUNGANA NA ILEMELA KUMUUNGA MKONO MAKAMU WA RAIS JUU YA UTUNZAJI NA UHIFADHI MAZINGIRA

Benki ya Diamond Trust Bank DTB mkoa wa Mwanza imeungana na Halmashauri ya manispaa ya Ilemela katika kumuunga mkono makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Samia Suluhu juu ya Utunzaji na Uhifadhi wa Mazingira kwa kufanya Usafi, kugawa miche elfu Tatu na mia tano na kisha kuipanda miche hiyo kuzunguka uzio wa manispaa ya Ilemela, hifadhi ya barabara ya Buwelu kuelekea wilayani na viwanja vya manispaa tukio lilipambwa na kauli mbiu ya ‘ MAZINGIRA YETU, MAISHA YETU ’


Akizungumza katika tukio hilo mgeni rasmi na mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula amesema kuwa tukio la ufanyaji usafi, upandaji miti na utunzaji wa mazingira kwa Ilemela limekuwa tukio endelevu kwani hata siku ya kuzinduliwa kwa uzio wa manispaa hiyo na makamu huyo wa Rais alisisitiza na kuelekeza kutunza mazingira na kupanda miti huku yeye mwenyewe akianza kwa kupanda mti ndani viwanja ya manispaa huku akiwashukuru Benki ya DTB kwa namna walivyojitoa katika kuhakikisha mazingira yanatunzwa na kulindwa sanjari na uoteshaji wa miti mipya waliyoitoa


‘… Ndugu zangu mtakumbuka siku ya uzinduzi wa ujenzi wa uzio wa halmashauri hii Mhe Makamu wa Rais alisisitiza pia juu ya utunzaji wa mazingira na upandaji miti nayeye mwenyewe alipanda mti kama ushahidi kwa hiyo jambo tunalolifanya leo ni kuendeleza kile ambacho amekuwa akikisimamia kama mlezi na hivi karibuni pale Dodoma eneo la mzakwe amezindua kampeni ya kubadili hali ya mazingira, Kwetu sisi ni namna ya kuendeleza mazingira yetu na bahati nzuri wenzetu wa DTB Benki wamejitokeza na tumekubaliana nao mpango huu tutakuwa tukiuendeleza mwaka hadi mwaka …’ Alisema


Aidha tukio hilo pia lilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira Mhe Kange Lugola ambapo amewataka wananchi kuacha kukata miti kwa kisingizo cha kupata nishati ya mkaa huku akiwaasa juu ya utumiaji wa nishati mbadala iliyorafiki wa mazingira mfano wa gesi sanjari na kuelezea hatua mbalimbali Serikali inazozichukua kupambana na uharibifu wa mazingira nakuzitaka halmashauri zote nchini kuzisimamia sheria za mazingira na uimarishwaji wa kamati zake kwa ngazi zote na kuahidi kuitembelea tena Ilemela mapema Januari, 2018

Nae mwakilishi kutoka Benki ya DTB Ndugu Sylvester Bahati amesema kuwa Benki yake imekuwa ikishirikiana na Serikali katika kusaidia wananchi kwa kutoa huduma mbalimbali ikiwemo huduma za afya na Elimu hivyo zoezi la utoaji na upandaji miti ni muendelezo wa utoaji wa huduma kwa jamii kama inavyofanya maeneo mengine huku akiahidi kuendeleza mpango huo kwa kushirikiana na manispaa ya Ilemela


Akihitimisha Mstahiki Meya wa manispaa ya Ilemela Mhe Renatus Mulunga ameeleza juu ya umuhimu wa kutunza mazingira huku mkurugenzi wake John Wanga akiahidi kutekeleza maelekezo yote waliyoyatoa juu ya utunzaji mazingira na kushukuru kwa ushiriki wa viongozi hao katika zoezi hilo la kuhakikisha mazingira yanatunzwa.

Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.