Mstahiki meya wa manispaa ya Ilemela ameongoza mkutano maalum wa baraza la madiwani kwa ajili ya kupitia na kujadili taarifa ya ufungaji wa hesabu za mwisho za mwaka wa fedha 2023/2024
Akiwasilisha taarifa hiyo kwa niaba ya mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela, Mweka Hazina Julius Ndyanabo, amesema kuwa taarifa za hesabu za halmashauri zinahusisha maeneo manne ambayo ni; taarifa za halmashauri, ripoti ya mahesabu ya mwaka 2023/2024 , taarifa za hesabu kwa mwaka 2023/2024 zikihusisha mizania ya hesabu, mapato na matumizi, mtiririko wa fedha, na mabadiliko ya urali wa mizani na eneo la nne ni mchanganuo wa taarifa ya hesabu za mwisho.
Nao waheshimiwa madiwani katika nyakati tofauti, wamepongeza kwa namna taarifa ilivyoandaliwa, huku wakisisitiza kuongeza kasi katika suala zima la ukusanyaji na usimamizi wa mapato ya halmashauri.
Ufungaji wa hesabu za mwisho wa mwaka wa fedha ni takwa la kisheria chini ya sheria ya serikali za mitaa yam waka 1982 kifungu na 40 (pamoja na marekebisho yam waka 2000) kwamba halmashauri zinapaswa kuandaa hesabu na kuwasilisha kwa mkaguzi na mdhibiti mkuu wa hesabu za serikali (CAG) kabla au ifikapo tarehe 30/09 ya kila mwaka.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.