Baraza la madiwani la Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela limejadiri taarifa za utekelezaji wa shughuli za maendeleo zilizopo katika kata zote 19 zinazounda Manispaa hiyo.
Wakichangia mada kwa nyakati tofauti waheshimiwa madiwani wamezungumzia mambo mbalimbali ikiwemo changamoto za miundo mbinu ya barabara , masoko, umeme na maji katika kata zao sambamba na malipo ya fidia kwa wananchi kwenye maeneo ambayo serikali ina mpango wa kuweka huduma za jamii.
"Ukusanyaji wa mapato kwetu ni kipaumbele, Halmashauri bila kukusanya mapato haiwezi kujiendesha. Tunayo miradi mingi ya kujenga na kukamilisha bila pesa hayo yote hayatawezekana. " Amesema Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Mhe.Renatus Mulunga.
Nae Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bi.Ummy Wayayu amepokea maelekezo na maoni yote yaliyotolewa na madiwani hao huku akiwaomba madiwani kutoa ushirikiano wa kutosha katika kufanikisha malengo yao kwa kila mmoja kuanisha kitu muhimu kwenye kata zao ili vianze kufanyiwa kazi kwa umuhimu wake .
Mkutano wa baraza la madiwani kujadili taarifa za utekelezaji kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2023/2024 inayoanzia mwezi Aprili hadi Juni utafanyika kesho Agosti 1, 2024 kwa ajili ya kujadili kwa kina na uwazi zaidi taarifa hizo ambapo wadau mbalimbali wa maendeleo,wataalam kutoka taasisi mbalimbali na wananchi wote ni wahusika.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.