Baraza la Madiwani la mji kati Mkoa wa Kusini Zanzibar limefanya ziara ya mafunzo katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mnamo tarehe 09 mwezi wa 9 2023 ikiongozwa na Mwenyekiti wao Mhe. Said Hassan Shaaban.
Lengo la ziara hiyo ilikuwa ni kujifunza masuala mbalimbali ya uendeshaji wa Shughuli za Halmashauri hususan suala la ukusanyaji wa Mapato.
Sambamba na hilo wamejifunza juu ya masuala ya Sheria ndogo,uendeshaji wa vikao vya halmashauri, utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na usimamizi wa leseni za Biashara.
Wakishukuru mara baada ya kuhitimisha ziara hiyo kwa kutembelea stendi ya mabasi Nyamhongolo,wamepongeza kwa hatua mbalimbali ambayo Ilemela imepiga na kuahidi kwenda kuyafanyia kazi waliojifunza ili Halmashauri yao nayo isonge mbele.
" Sisi kutoka zanzibar tumejifunza mengi ambayo yatatusaidia huko kwetu tutaenda kuyafanyia kazi pia tutaenda kuutangaza ukarimu wenu watu wa Ilemela", Aliseme Mhe.Said Shabaan Mwenyekiti wa Baraza la mji Kati.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.