Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela mkoani Mwanza inatarajia kutekeleza mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami.
Barabara ambazo zitajengwa ni tatu zenye jumla ya urefu wa kilomita 12.1 nazo ni barabara ya Sabasaba-Kiseke-Buswelu (kilomita 9.7), Isamilo-Mji mwema-Bigbite(Kilomita 1.2) na Makongoro Junction-Mwaloni(Km 1.2).
Ujenzi wa barabara hizi utatekelezwa na mradi wa mpango mkakati wa uendelezaji miji Tanzania(TSCP) kwa kutumia fedha za nyongeza awamu ya pili kupitia mkopo wa benki ya Dunia.
Raphael Mfuru ambae ni Mratibu wa TCSP kwa upande wa Ilemela, amesema kuwa hadi sasa jumla ya shilingi za kitanzania 432,868,238 kati ya shilingi 636,626,000 ambazo zimelipwa fidia kwa wananchi 116 kati ya 170 ili kuwawezesha kupisha eneo ambalo barabara itapita.
Aidha amewashukuru wananchi 42 ambao wamejitolea maeneo yao bure kwa ajili ya kupisha utekelezaji wa ujenzi wa barabara ya Sabasaba-Kiseke-Buswelu.
Ujenzi wa barabara hizi unatarajia kuanza kutekelezwa mapema mwezi Juni mwaka huu 2018 mara baada ya kukamilika kwa taratibu za zabuni.
Sehemu ya barabara ya Sabasaba-Kiseke-Buswelu inavyoonekana kwa sasa kabla ujenzi wa barabara hiyo kuanza
Timu ya wataalam kutoka benki ya dunia, Ofisi ya Rais TAMISEMI pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela wakikagua barabara zitakazojengwa kwa kiwango cha lami
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.