Mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe.Dkt.Angeline Mabula amekabidhi mradi wa ujenzi wa barabara ya Ilemela - Mahakamani iliyopo kata ya Ilemela kwa mkandarasi JASSIE & COMPANY LIMITED (JASCO) kuanza kujengwa mara moja lengo ikiwa ni kuwapunguzia changamoto ya usafiri wananchi wa Ilemela na maeneo mengine.
" ..Hapa imetengwa shilingi milioni 374.95 kukamilisha mradi huu tuna kila sababu ya kumshukuru na kumuunga mkono Rais wetu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kazi nzuri anayoendelea nayo..." Amesema Mhe.Mabula
Akitoa taarifa ya mradi huo Meneja wa TARURA wilaya ya Ilemela Mha.Sobe amesema barabara ya Ilemela - Mahakamani ina jumla ya urefu wa kilomita 1.2 na kwa utekelezaji wa awamu ya kwanza utafanyika kwa kipande cha mita 500 sawa kilomita 0.5 kwa kiwango cha lami.
"Utekelezaji wa mradi mzima utagharimu kiasi cha shilingi 374,950,430 fedha iliyotokana na tozo " fuel levy fund " kwa mwaka wa fedha 2024/2025 ,mradi unatarajiwa kutekelezwa kwa kipindi cha miezi sita ambapo kazi zitakazofanyika ni pamoja na ujenzi wa mitaro mita 800,makalvati matatu na uwekaji wa alama na michoro barabarani.
Nae mwakilishi wa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ndugu Jeremiah Lugembe amesema kukamilika barabara hiyo kutavutia biashara na uwekezaji maeneo hayo na kuongeza pato la mwananchi mmoja mmoja na hatimae kukupa mapato ya Manispaa ya Ilemela.
Mhe.Mabula amewataka wananchi hao kubeba umiliki wa mradi huo na kushirikiana katika kuzipa unafuu barabara nyingine za mitaa ambazo bado hazijafikiwa na TARURA kwa ajili ya matengenezo.
Gaudencia Anithet ni mmoja wa wafanyabiashara wa soko la Ilemela ambako barabara hiyo inapita, amesema itakuwa fursa nzuri kwa wao kufikisha bidhaa zao sokoni kwa haraka na urahisi na kwamba anatarajia wateja wataongezeka.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.