Taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa TAKUKURU Ilemela imetoa elimu ya rushwa kwa Asasi zisizo za kiserikali zinazojihusisha na sekta mbalimbali ikiwemo elimu,afya, kilimo,teknolojia ya habari na mawasiliano na haki za binadanamu zinazofanya kazi zake ndani ya Manispaa ya Ilemela ikiwa ni sehemu ya kuleta uelewa wa pamoja juu ya misingi ya utawala bora na sheria.
Akizungumza wakati wa jukwaa la asasi zisizo za kiserikali (NGOs) kujadili taarifa zao za utekelezaji katika robo ya nne ya mwaka wa fedha 2023/2024 Afisa wa TAKUKURU Bi.Doreen Ntongani amesema ni muhimu taasisi zote za umma kufahamu umuhimu wa misingi ya utawala bora.
Amefafanua kuwa taasisi za umma ni zote zinazojihusisha na utoaji wa huduma kwa jamii zinaweza kuwa za kiserikali au zisizokuwa za kiserikali na kuzitaka taasisi hizo kwa pamoja kufanya kazi kwa uwazi na uwajibikaji na kuepuka mazingira yoyote ya rushwa.
"..Rushwa ni kitu chochote cha thamani kinachotolewa kwa manufaa binafsi hasa kwa watu wenye mamlaka,kuishinda inahitaji wote tuungane na kuipinga "
Amewataka viongozi katika asasi hizo kuajiri wafanyakazi kwa uwezo wao na vigezo vinavyotakiwa na si kwa upendeleo wa namna yoyote kwa kuangalia kabila ,dini au vyuo walivyotoka huku akiwatahadharisha namna rushwa inavyoweza kuua uzalendo.
Akijibu swali la Vivian Kori Meneja wa asasi ya Fadhili Teens Tanzania alilohoji ugumu wa upatikanaji wa taarifa za taasisi za serikali Bi Doreen amesema ni haki ya kikatiba raia kupata habari na kuwataka wataalam wa asasi hizo kuhudhuria mikutano ya wazi kama vile mabaraza ya madiwani ambako taarifa zote za umma zinatolewa.
Jimmy Luhende ni Mwenyekiti wa asasi zisizo za kiserikali mkoa wa Mwanza yeye amewataka wakurugenzi wenzie kwenye asasi zao kuwa na mahusiano ya karibu na wataalam mbalimbali wa kiserikali ili kurahisisha mawasiliano baina yao.
Akihitimisha kikao hicho Msajiri wa asasi zisizo za kiserikali wilaya ya Ilemela ndugu Yusuph Onkwonkwo amezishukuru asasi zote kwa ushiriki wao huku akiwataka kuboresha zaidi taarifa zao za utendaji kutumia majukwaa ya aina hiyo kutoa maoni na mawazo mapya ili kufanya kazi zao kuwa bora zaidi.
|
|
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.