Aliyekuwa mgombea Ubunge kupitia tiketi ya Chama cha Mapinduzi, Angeline Sylvester Mabula ameibuka mshindi katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 uliofanyika tarehe 28 mwezi wa Kumi.
Akitangaza matokeo hayo kwa mamlaka aliyopewa, Msimamizi wa uchaguzi Jimbo la Ilemela John Wanga, amemtangaza rasmi Ndugu Angeline Mabula kuwa Mbunge wa Ilemela kwa awamu ya pili ambae ameshinda kwa kura 147,724 kati ya kura halali 176,051 zilizopigwa ambayo ni sawa na asilimia 84 ya kura zote.
Wagombea ubunge wengine waliokuwa katika kinyang’anyiro hicho cha uchaguzi kwa nafasi ya ubunge katika jimbo la Ilemela ni pamoja na CHADEMA ambae amepata kura 24,022 sawa na asilimia 14, ACT –Wazalendo kura 2761 sawa na asilimia 2, ADC kura 560 (0%), NRA kura 218 (0%), DEMOKRASIA MAKINI kura 664(0%) NA DP ambao wamepata kura 102 (0%)
Kwa upande wa udiwani Chama cha Mapinduzi kimeibuka kidedea katika kata zote 19, ambapo kati ya kata hizo, Madiwani kutoka kata nne za Kayenze, Kahama, Nyamhongolo na Nyakato walipita bila kupingwa na kata 15 ndizo zilishiriki uchaguzi huu
Vyama vilivyoshiriki uchaguzi kwa upande wa udiwani ni pamoja na CCM, CHADEMA, ACT wazalendo , CUF, ADC, NCCR Mageuzi, na UDP
Idadi ya wapiga kura walioandikishwa walikuwa 302,552 kutoka kata 19 waliojiandikisha kupiga kura katika vituo 795 ambapo jumla ya wananchi waliopiga kura ni 177,677, kura halali ni 176,051 na kura zilizokataliwa ni 1,626.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.