• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

AFISA MAENDELEO YA JAMII AVITAKA VIKUNDI KUZINGATIA SHERIA NA TARATIBU ZA MIKOPO

Posted on: April 28th, 2020

Vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu vimetakiwa kuhakikisha kuwa vinazingatia sheria  na taratibu za fedha zinazotolewa na Halmashauri baada kutenga asilimia kumi ya mapato yake ya ndani wakati wa  zoezi la utoaji na urejeshaji wa mikopo.

Rai hiyo imetolewa na afisa maendeleo ya jamii wa manispaa ya Ilemela, Ndugu Sitta Singibala wakati akizungumza na viongozi wa vikundi vya vijana, wanawake na watu wenye ulemavu kutoka kata za wilaya hiyo ambapo amewataka kuzingatia utaratibu na sheria ya fedha ya mwaka 2019 inayoratibu zoezi la utoaji wa mikopo kwa vikundi kwa kuhakikisha wanatumia fedha zinazotolewa kwa kufanyia shughuli za kiuchumi zenye tija kwao na zenye kuwawezesha kurejesha mikopo hiyo bila vikwazo na kwa wakati.


“Kazi ya serikali ni kuwawezesha wananchi wake kuishi katika muelekeo sahihi na kupata nafuu ya maisha,mikopo hii ni zoezi endelevu hivyo ni lazima irejeshwe .Leo mmeitwa hapa kwa ajili ya kujaza mikataba na kukumbushwa sheria na taratibu za fedha hizi.Nyie ni viongozi wa vikundi vyenu elimu hii tunayowapatia hapa tunategemea iwafikie wanavikikundi wote.”Amesema.


Nae Afisa Maendeleo ya jamii Bi.Amina Bululu amewataka viongozi hao wa vikundi kuwatumia maafisa watendaji wa kata katika maeneo yao kwa changamoto zozote watakazokumbana nazo katika shughuli zao na wasikimbilie Wilayani kwa kila jambo.

“Watendaji wanao uwezo wa kutatua changamoto nyingi ikiwemo hizi za mikopo ya Halmashauri,una swali uliza kwake ikionekana ni jambo gumu linalohitaji ushiriki wa Maafisa Maendeleo ya jamii sisi tupo kwa ajili yenu”.Amesema.


Aidha Bi Florence Vedasto ambae ni Afisa maendeleo ya jamii mwandamizi ametoa maelekezo ya namna ya kurejesha fedha za mikopo hiyo na kuwataka viongozi wa vikundi kuwa makini katika benki wanayolipia na kutunza kumbukumbu“Ni muhimu kutunza risiti baada ya malipo kwani ndicho kithibitisho pekee kwamba pesa imelipwa.”Amesema.

Akizungumzia sheria ya fedha za mikopo ya mwaka 2019 ,Afisa Vijana wa Halmashauri ya Manispaa Bi.Lucy Matemba amesema endapo kikundi kitashindwa kurejesha kwa wakati sheria hiyo itakutaka ufikishwe mahakamani na ulipe gharama zote za mahakama na hatimae kufanya rejesho chini ya sheria.


“Mikopo hii haina riba ila mnatakiwa kurejesha  kama taratibu zinavyowataka mfanye.Hatuna sababu ya kuvutana hadi mahakamani au kutumia nguvu.Sera ya vijana izingatiwe hasahasa kwa vikundi vya vijana.Kama umri umepita jitoe au ubaki kama mshauri wa kikundi.Lengo ni vikundi vya vijana vibaki na uhalisia wake”Amesema.

Kwa kipindi cha kuanzia mwezi July 2019 hadi April 2020 halmashauri ya Manispaa ya Ilemela imetoa jumla ya kiasi cha Shilingi milioni 540 kwa vikundi 166 ambapo vikundi 126 ni vya wanawake, vikundi 32 ni vya vijana na vikundi 8 ni vya watu wenye ulemavu, ikiwa ni katika kutekeleza agizo la serikali la kutenga asilimia 10 ya mapato ya kila mwezi ya Halmashauri kwa ajili ya kuviwezesha vikundi hivyo.







Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • WALENGWA TASAF WAASWA KUENDELEA KUWEKEZA KATIKA VIKUNDI

    April 28, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.