Kata ya Kayenze ni miongoni mwa kata 19 zinazunda Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela. Ina jumla ya mitaa mitano, kaya 4,187, na idadi ya watu 17,201 wanaume 8,562 na wanawake 8,639 kwa mujibu wa sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022.Ina shule tatu za msingi na shule moja ya sekondari ambazo ni shule ya msingi Kayenze, Shule ya Msingi Bezi na Shule ya Msingi Chasubi pamoja na Shule ya Sekondari Kayenze.
KIUONGOZI NA KIUTENDAJI
Mheshimiwa mwenyekiti, Viongozi katika kata ya Kayenze ni kama ifuatavyo; Tunaye mhe. Issa Mwalukila Dida (Diwani) na Mwenyeviti wa serikali ya mtaa wa Iponyabugali. Wenyeviti wengine ni pamoja na Amos Mmbaga (Iseni), Daudi K. Malaji(Lutongo), Ramadhani Haruna Ramadhani (Bezi), na Yasin Haruna Chande mwenyekiti mtaa wa Kayenze, na mtendaji wa kata ni Mponeja Katemi
Kata ya Kayenze inazo shule tatu za msingi ambazo ni Chasubi, Kayenze na Bezi
Kata ya Kayenze kuna shule moja ya Sekondari ya Kayenze sekondari ambayo kwa sasa imefikisha kidato cha nne na itakuwa na jumla ya wanafunzi 1050 kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.