Utoaji wa huduma kwa jamii katika sekta hii ni pamoja na kutoa ushauri juu ya ufugaji bora, mafunzo kwa wafugaji, kutoa tiba na kinga, usafi na ukaguzi wa nyama, uwambaji bora wa ngozi, ujenzi wa mabanda bora ya mifugo, usimamizi na uangalizi wa shughuli za Majosho na Malambo. Mazao ya chakula yatokanayo na mifugo ni Maziwa, Nyama na Mayai.
Wilaya ina Ng’ombe wa asili wapatao 24,156, Ng’ombe wa maziwa 15,898, Mbuzi wa asili 9,903, Mbuzi wa maziwa 348, Kondoo 2651, Punda 216, Mbwa 11734, Paka 1495, Kuku Wa asili 73,581, Kuku wa mayai 21,206, Nguruwe 51,714 na Bata 460.
Miundo mbinu inayopatikana katika Halmashauri ni pamoja na Majosho matano, Malambo nane, Machinjio mawili na vibanio vitano pamoja na Kituo cha uhamilishaji Mifugo kimoja.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.