Katika kuboresha maeneo kwa ajili ya Wafanyabiashara ndogondogo, Halmashauri inajumla ya wafanyabiashara wadogo wadogo 4,072 ambapo uongozi wa Wilaya umeweza kufanya vikao na viongozi wa wafanyabiashara hao katika masoko mbalimbali yaliyoko. Wilaya imewaelimisha kutekeleza mambo yafuatayo;
(a) Kuenedelea kuwafahamisha wafanyabiashara wadogo wadogo azma ya Serikali katika kuendelea kuandaa na kuboresha miundo mbinu ya maeneo yao ya kufanyia biashara;
(b)Kuendelea kufanya mazungumzo na kuwafahamisha wafanyabiasha maeneo rasmi wanayotakiwa kufanyia biashara zao;
(c)Kuwahamasisha wafanyabiasha kuhusu utunzaji wa mazingira, ikiwa ni pamoja na kutokufanya shughuli zozote au biashara maeneo yasiyoruhusiwa;
(d)Kuendelea kujenga umoja na mshikamano baina ya wafanyabiashara, ili kusaidia kutambua watu wasio na nia njema wenye lengo la kuvuruga Amani ya Nchi yetu;
(e)Halmashauri pia imewasaidia wafanyabiashara katika masoko katika kuandaa na kusajili katiba na hadi hivi sasa masoko yote yana Katiba
(f)Wafanyabiashara katika Masoko ya Kirumba na Kiloleli wamepatiwa elimu ya Ujasiriamali iliyokuwa inaendeshwa bila malipo
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.