• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya Mara kwa Mara |
    • Barua Pepe za Watumishi |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA MANISPAA YA ILEMELA

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dhima na Dira
    • Maadili ya Msingi
      • Mikakati ya MSM
    • Mikakati ya MSM
  • Utawala
    • Muundo wa Taasisi
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika
      • Fedha na Biashara
      • Mipango, Takwimu na Ufuatiliaji
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Elimu ya Sekondari
      • Maji
      • Ufugaji na Uvuvi
      • Ardhi na Mipango Miji
      • Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii
      • Ujenzi
      • Elimu ya Msingi
      • Mazingira na Usafishaji
    • Vitengo
      • Kitengo cha Sheria
      • Kitengo Cha Nyuki
      • Kitengo cha Uchaguzi
      • Kitengo cha ukaguzi wa ndani
      • Kiengo cha Ugavi
      • Kitengo cha Uhusiano na TEHAMA
    • Kata
      • Sangabuye
      • Nyasaka
      • Buswelu
      • Nyamhongolo
      • Kayenze
      • Bugogwa
      • Shibula
      • Ilemela
      • Kahama
      • Kiseke
      • Pasiansi
      • Kawekamo
      • Ibungilo
      • Nyamanoro
      • Buzuruga
      • Mecco
      • Nyakato
      • Kirumba
      • Kitangiri
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Uvuvi
    • Ufugaji
    • Kilimo
    • Viwanda
    • Michezo
  • Huduma zetu
    • Elimu
    • Afya
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za Watumishi
  • Madiwani
    • Orodha ya wah. wabunge na madiwani
    • Kamati za kudumu za halmashauri
      • Fedha na Uongozi
      • MipangoMiji na Mazingira
      • Uchumi Afya na Elimu
      • UKIMWI
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi Iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Huduma Kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Taarifa
    • Fomu
    • Miongozo Mbalimbali
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Video
    • Hotuba

Mgogoro wa ardhi Kigoto wahitimishwa rasmi

Posted on: March 4th, 2021

Mgogoro wa ardhi katika eneo la Kigoto kata ya Kirumba uliodumu muda mrefu kwa zaidi ya miaka thelathini iliyopita umehitimishwa rasmi na Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya makazi Mhe. William Lukuvi alipogawa ankara za malipo kwa wananchi wa eneo hilo la Kigoto.


Waziri Lukuvi akihutubia wananchi wa kigoto amesema kuwa amekuja kuhitimisha mgogoro huo rasmi kwa kuwakabidhi wananchi hao ankara za malipo ili waweze kuandaliwa hati ya miaka 99 na hii ikiwa ni baada ya uamuzi wa Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuagiza kuwa wananchi hao wamilikshwe ardhi.

Aliongeza kwa kusema kuwa jumla ekari 56 za serikali zimetolewa kwa wananchi wa eneo la Kigoto huku jumla ya ekari 16 zikiwa zimebaki katika Jeshi la polisi kwa kufuata maelekezo ya Mhe. Rais.


Akigawa ankara hizo za viwanja 600 kwa wananchi wa Kigoto, ameitaka Idara ya ardhi kuhakikisha kuwa mwananchi anapolipia gharama za umilikishaji anapatiwa hati yake ndani ya siku 7.

Aidha amewahimiza wananchi kuhakikisha wanafanya malipo yaliyoainishwa katika ankara za malipo ili waweze kupatiwa hati na amesema kuwa angefurahi iwapo wananchi wote ndani ya miezi 3 wawe wamelipia na kumiliki hati zao ili ziweze kuwasaidia kujikwamua kiuchumi.


Akifikisha salam za Mhe. Rais na kusema kuwa, Rais Magufuli amewataka wananchi wa eneo hilo kuondoa hofu kwani eneo hilo la serikali la ukubwa wa ekari 56 limetolewa bure kwa wananchi, na gharama zitakuwa ni kwa ajili ya kulipia umilikishwaji tu na si vinginevyo.


Pamoja na hayo Waziri Lukuvi amewataka wananchi kuacha kuvamia maeneo ya serikali kwa  kudhani kuwa watakuja kumilikishwa na kuzitaka taasisi zote za serikali kuhakikisha wayalinda maeneo yao yasivamiwe kwani ni jukumu lao.


Nae Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Mhe Angeline Mabula amemshukuru Mhe. Rais kwa kutatua mgogoro huu uliokuwa ukileta adha kubwa kwa wananchi kwani wananchi walishindwa kupata huduma mbalimbali za kijamii


Kupitia wananchi wa Kigoto Mhe Mbunge amewaahidi wananchi wa Ilemela kuwa atahakikisha changamoto za migogoro ya ardhi zinatatuliwa na kuisha kabisa.


Mkuu wa Wilaya ya Ilemela, amemshukuru Rais kwa kitendo chake cha kuwajali wanyonge na kusema kuwa kitendo cha kuwapa bure wananchi ekari 56 inaonyesha ni namna gani Rais anawajali wananchi wanyonge.


“Ekari 16 zimebaki kwa jeshi la polisi huku ekari 56 zikienda kwa wananchi, hali hii inadhihirisha kuwa Mhe. Rais anatetea wananchi wanyonge”, Alisema.


Mgogoro huu uliohusisha jeshi la polisi na wananchi ulianza kutatuliwa na serikali kuanzia mwaka 2017 ambapo ulipitia katika hatua mbalimbali chini ya Wizara ya ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi.





Matangazo

  • TANGAZO LA AJIRA YA KAZI MTENDAJI WA MTAA March 03, 2021
  • Matokeo Darasa la Saba2020 November 23, 2020
  • Orodha ya Majina ya wanafunzi wavulana na wasichana waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2021 shule za kutwa December 19, 2020
  • Orodha ya majina ya wanafunzi waliochaguliwa kujiunga na kidato cha kwanza 2021 -Mahitaji maalum December 19, 2020
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Mganga Mkuu Ilemela awataka wadau kuendelea kuunga mkono jithada za serikali

    April 15, 2021
  • Wananfunzi wajengewa uwezo kupinga vitendo vya ukatili na unyanyasaji

    March 09, 2021
  • Mgogoro wa ardhi Kigoto wahitimishwa rasmi

    March 04, 2021
  • Wataalam wa elimu, afya na ustawi wa jamii wajengewa uwezo wa kupambana na vitendo vya ukatili

    February 23, 2021
  • Angalia zote

Video

Madiwani Ilemela waapishwa /wampata meya wao
Video zaidi

Ukurasa wa Karibu

  • Kuhakiki Taarifa za Mpiga Kura
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip
  • Maombi ya leseni ya biashara

Kurasa zinazofanana

  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza
  • Tovuti Kuu ya serikali

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Wasiliana nasi

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Anuani ya Posta: 735 MWANZA

    Simu: + 255 736 200910

    Simu:

    Barua Pepe: md@ilemelamc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Ramani ya Tovuti

Haki Miliki 2019 Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.Haki zote zimeifadhiwa