Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela kama zilivyo mamlaka zingine za serikali za mitaa inatekeleza mradi wa mfumo wa anwani za makazi na postikodi kama ilivyoelekezwa na Mhe. Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassim Majaliwa Kasimu wakati akizindua Mradi huu tarehe 14/09/2016.
Zoezi hili litatekelezwa kwa awamu mbili ambapo kwa awamu ya kwanza zoezi hili katika Manispaa ya Ilemela litafanyika katika jumla ya Kata 8 ambazo ni Kirumba, Nyamanoro, Pasiansi, Nyakato, Mecco, Buzuruga, Buswelu na Ilemela ambazo zina jumla ya Mitaa 56.
Kukamilika kwa zoezi hili la uwekaji wa mfumo wa anwani za makazi na potikodi utasaidia na kurahisisha;Utambuzi wa maeneo wanayoishi wananchi kwa ajili ya kurahisha huduma, Utoaji wa huduma kwa wananchi kwa urahisi baada ya kutambulika mf. Huduma za afya, Posta,Benki, Utoaji wa taarifa za kuzuia uhalifu kwa haraka mf. Ujambazi, wizi pamoja na utoaji wa taarifa za majanga yanapotokea mfano majanga ya Moto
Zoezi hili la uwekaji wa anwani za makazi na postikodi linaendeshwa na Manispaa ya Ilemela, kwa kushirikina na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi Na Mawasiliano pamoja na ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, ambapo hadi sasa Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela imepokea nguzo 579 na mbawa 1145 kwa ajii ya utekelezaji wa zoezi hilo kwa awamu ya kwanza.
Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela
Postal Address: 735 MWANZA
Telephone: + 255 736 200910
Mobile:
Email: md@ilemelamc.go.tz
Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.