• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

ZAIDI YA SHILINGI BILIONI 18 ZA KITANZANIA KUJENGA BARABARA MANISPAA YA ILEMELA

Posted on: June 8th, 2018

Zaidi ya shilingi bilioni 18 za kitanzania zinatarajia kutumika katika ujenzi wa barabara za Manispaa ya Ilemela kwa kiwango cha lami.

Hayo yamebainishwa leo tarehe 08/06/2018 na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Ndugu John Wanga kwenye hafla fupi ya utiaji saini mkataba wa ujenzi wa barabara kati ya Manispaa ya Ilemela na kampuni ya Synohydro Ltd ya China.

Ujenzi wa barabara hizo zenye jumla ya urefu wa kilomita 12.1 utahusisha barabara ya Sabasaba-Kiseke-Buswelu(Kilomita 9.7), Isamilo-Mjimwema(Bigbite, Kilomita 1.2)makutano ya barabara ya Makongoro-Mwaloni Kirumba(Kilomita 1.2) halikadhalika pamoja na uwekaji wa taa za barabarani  na mabirika ya kukusanyia taka.

Akitoa neno la shukrani  katika hafla ya utiaji saini mkataba huo, Mstahiki meya wa Manispaa ya Ilemela, Mhe Renatus Mulunga amesema kuwa hadi sasa shilingi za kitanzania milioni 436 kati ya shilingi milioni 636 zimelipwa fidia kwa wananchi kutoka katika mapato ya ndani ya halmashauri .

Mwakilishi wa kampuni ya Sinohydro Ndugu Jia Bin amesema kuwa ujenzi wa barabara unatarajiwa kuanza Juni 15 mwaka huu, ambapo  utatekelezwa ndani ya miezi 15 na kuahidi kuwa watahakikisha wanamaliza kwa wakati uliokusudiwa na utajengwa kwa ubora wa hali ya juu.

Baadhi ya wananchi waliofika kushuhudia utiaji saini mkataba wa barabara hizo wamepongeza hatua hiyo na  kusema kuwa, kukamilika kwa ujenzi wa barabara hizi kutasaidia kurahisisha usafiri kwa wananchi na mizigo hususani kata ambazo mradi unapita pamoja na kuimarisha huduma za kiuchumi na kijamii kama vile shule, hospitali na masoko.

Mradi wa ujenzi wa barabara hizi unagharimiwa na fedha za mkopo kutoka Benki ya Dunia chini ya mradi wa uendelezaji Miji na Majiji “Tanzania Strategic Cities Project”.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilemella Renatus Mulunga (Aliyeketi) akitia saini

 mkataba wa ujenzi wa barabara za Manispaa ya Ilemela


Mkurugenzi John Wanga (mwenye tai) akitia saini mkataba wa ujenzi huku akishuhudiwa na waalikwa


Mstahiki Meya Renatus Mulunga (Katikati) pamoja na mwakilishi wa kampuni ya synohydro (Upande wa kushoto) Ndg. Jia Bin

pamoja na Mkurugenzi  John Wanga(Upande wa kulia)wakipongezana mara baada ya kusaini mkataba 

Kutoka kushoto ni mwakilishi wa kampuni ya Sinohydro Corporation Jia Bin, 

Mstahiki Meya Manispaa ya Ilemela Renatus Mulunga pamoja na 

Mkurugenzi wa Manispaa hiyo John Wanga wakionyesha mkataba wa makubaliano kwa wananchi

Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.