• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

WANANCHI WATAKIWA KUTUMIA FURSA YA KLINIKI YA ARDHI KUPATA HATI

Posted on: January 17th, 2024

Ikiwa ni siku ya saba (7) toka kuanza kwa kliniki ya ardhi ndani ya Manispaa ya Ilemela, Katibu Tawala wa Wilaya ya Ilemela Wakili Mariam Msengi, kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Ilemela amekabidhi hati 100 kati ya hati 376 ambazo zimekwishaandaliwa  kwa wanachi wanaomiliki ardhi ndani ya Manispaa ya Ilemela.


Akizungumza wakati wa hafla fupi ya kukabidhi hati hizo, Wakili Mariam amewataka wananchi kutumia fursa hii ya kliniki ya ardhi  kwa ajili ya utatuzi wa  changamoto yoyote ile ya ardhi  inayopelekea kushindwa kupata hati sambamba na kuwataka kuwa mabalozi wazuri  kwa wananchi wanaopitia changamoto za ardhi kwani mahali hapa ni salama na sahihi kwao.


“Zoezi hili ni kutokana na maelekezo ya Mhe Rais, ambapo alielekeza kusogeza huduma kwa wananchi wetu, na huduma imesogezwa clinic hii itakuwa ni endelevu  hivyo mwenye changamoto yoyote ile ya ardhi ikihusisha kupata hati, migogoro katika maeneo yetu ambayo inapelekea kushindwa  kupata hati hapa ni eneo sahihi” Alisema Wakili Mariam


Akitoa taarifa ya utendaji kazi wa kliniki hiyo Afisa ardhi mteule wa Manispaa ya Ilemela Bi.Grace Masawe amesema zaidi ya hatimiliki 376 zimeandaliwa na kusajiliwa,  migogoro 93 imepokelewa huku migogoro 23 katika hiyo ikipatiwa ufumbuzi wa kudumu na migogoro mingine ikiwa ipo katika hatua mbalimbali za kutatuliwa, ambapo wananchi 211 wamesikilizwa ikiwa ni pamoja na kutoa elimu juu ya masuala mbalimbali ya ardhi.


Nae kamishna wa Ardhi Msaidizi Mkoa wa Mwanza Bi.Happiness Mtutwa amewataka wananchi kufika ofisi za ardhi na kupata huduma wanazohitaji kwani wapo tayari kuwahudumia na kuwaondolea kero zinazowakabili.


“Tuna utayari na tupo tayari kuwahudumia wananchi na tunatamani asiwepo mwananchi wa Manispaa ya Ilemela /Mkoa wa mwanza anaelalamika kuhusiana na kutopewa huduma zetu ipasavyo au kutopata hati kwa wakati”.Alisema Bi Mtutwa


" Serikali ya awamu ya sita ipo kazini kutatua kero na shida za wananchi iwapo mwananchi umehudumiwa na hujaridhika fika ofisini na iwapo unazungushwa toa taarifa utapata haki yako,Ni matamanio yangu,  zoezi hili la kliniki ya ardhi lifanyike kila robo mwaka ndani ya Manispaa yetu ili tuweze kuwafikia wananchi wengi zaidi na kutatua kero nyingi kwa muda mfupi." Amesema Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Adv.Kiomoni Kibamba.


Wananchi ambao wamefika kwa ajili ya kupata hati wamefurwahishwa na zoezi hili huku wakiishukuru Serikali na kusema kuwa limewarahishia kupata hati ndani ya muda mchache tofauti na ilivyokuwa hapo awali.Huku wakiwataka wananchi  wenzao kuacha kukaa na kero na kuanza kufuatilia migogoro hiyo


“Kuanzia sasa hivi hati zitatoka, wenye migogoro itakwisha tusikae nyumbani kwa kuwaza kuwa ukifika utapigwa tarehe sasa hivi hamna cha tarehe mambo yako wazi kabisa wananchi tuamke nimefurahi sana kupata hati” Amesema Bi Priscila Desderi Mato mkazi wa Nyambiti Buzuruga


Elizabeth Magiri ni mkazi wa kata ya Nyasaka yeye anashukuru uongozi wa Ilemela kwa kuandaa huduma hiyo iliyomuwezesha kupata hati yake kwa muda mfupi kwani ni ulinzi wa kudumu wa ardhi yake


“Nilipigiwa simu kuja kuchukua hati ya kiwanja kilichopo Ilemela, ikiwa ni muda mfupi baada ya kufanya malipo na nikaambiwa kuichukua kwa kamishna tarehe 24 lakini nashangaa kabla ya tarehe 24 nimeipata hati yangu”  Alisema Paul Bruno ambae ametokea Wilaya ya  Ukerewe kata ya Bukindo,


Zoezi hili la kliniki ya ardhi litahitimishwa siku ya Ijumaa tarehe 19 Januari 2024, hivyo wananchi wametakiwa kuwasilisha nyaraka zao kwa ajili ya kuandaliwa hati miliki sambamba na kufika ofisi za Manispaa kuchukua hati zao.



Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.