• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

WANANCHI ILEMELA WAASWA KUPANDA MITI

Posted on: April 26th, 2023


Wananchi wa Ilemela wameaswa kutunza mazingira yao kwa kupanda miti mingi bila kuchoka kwa kuzingatia faida zake na ikiwa ni moja ya njia ya kupambana na mabadiliko ya tabia nchi sambamba na kufanya mazingira kuwa ya kuvutia zaidi.

Hayo yamezungumzwa na Afisa misitu wa Manispaa ya Ilemela Ndalahwa Bucheye wakati akitoa elimu juu ya namna bora ya kupanda miti na faida kwa wananafunzi na baadhi ya wananchi waliojitokeza kuadhimisha kumbukizi ya miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar inayoadhimishwa nchini kila tarehe 26 Aprili ya mwaka tangu Muungano huo ulipofanyika mnamo mwaka 1964 kupitia zoezi la upandaji miti lililofanyika katika shule mpya ya sekondari Igogwe iliyopo kata ya  Bugogwa .


"Miti pia ni chanzo cha kukuza uchumi kutegemea na aina ya mti uliopanda,kama ni ya mbao utavuna na kuuza mbao na kama ni ya matunda yatauzwa na kutumika kama chakula nyumbani ,tunapopanda tuzingatie upandaji wa kitaalam ili kupata matokeo chanya ..." amesema Bucheye


Nae Alex Julius ambaye ni Mhifadhi wa misitu kutoka mamlaka ya misitu Tanzania (TFS) Ilemela amesema ni muhimu kwa wananchi kuelewa faida za miti kwa maisha ya binadamu na hapo ndipo wataona umuhimu wa kuitunza.


"Tunatumia siku hii maalum kufikisha ujumbe kwa jamii na kuihamasisha katika suala zima la upandaji miti,utunzaji na usimamizi wake ili tuwe na matumizi endelevu ya rasilimali zetu za misitu..."amesema Alex


Jumla ya miti 300 iliyotolewa na TFS ya aina mbalimbali ya mbao,vivuli na matunda kama michungwa,mapera na miparachichi imepandwa shuleni hapo huku msisitizo ukitolewa juu ya utunzwaji wake.


Helena Samwel ni mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika shule hiyo yeye anashukuru uongozi wa Manispaa kwa kuchagua kupanda miti Igogwe sekondari na kuahidi kuwa yeye na wenzake kuwa mabalozi wazuri kwa jamii juu ya masuala ya utunzaji wa mazingira na upandaji miti.

Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.