• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

RC MAKALLA AIPONGEZA ILEMELA UKAMILISHAJI WA MRADI WA BOOST

Posted on: September 14th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe CPA Amos Makalla ameipongeza Manispaa ya Ilemela kwa kukamilisha ujenzi wa miundombinu ya elimu msingi kupitia mradi wa BOOST na kusema kuwa ameridhishwa na utekelezaji wa mradi huo.


Mhe.CPA Amos Makala ametoa pongezi hizo wakati wa hafla ya makabidhiano ya ukamilishaji wa miradi wa BOOST iliyofanyika tarehe 13 Septemba 2023, ambayo ilienda sambamba na .uzinduzi wa Shule mpya ya Msingi ya Buteja ambayo nayo  imejengwa kwa fedha za BOOST  


Akiongea na wananchi waliofika kushuhudia makabidhiano hayo, amesema kuwa katika Mkoa wa Mwanza Ilemela imekuwa ya kwanza kukabidhi mradi huu wa BOOST na kusema ina maanisha Ilemela inazungumza lugha moja, ameongeza kusema kuwa amekagua madarasa na ameridhishwa nayo.


“Ilemela mmekuwa wa kwanza kukamilisha na kukabidhi mradi huu wa BOOST kwa Mkoa wa Mwanza,maana yake hapa chama na serikali lugha yenu ni moja.Niwashukuru kwa kazi nzuri mliyofanya, nimeenda kwenye madarasa nimeona madawati mazuri nimeona hadi meza na kiti ch mwalimu nimepita sehemu nyingi sijawahi kuona na nimeliona Ilemela kwa mara ya kwanza”, alisema Mhe Makalla


Sambamaba na hilo CPA Makalla amesema kuwa Serikali imetoa fedha nyingi ya ujenzi wa miundombinu ya elimu mkoani Mwanza, hivyo amewataka wazazi, walezi, walimu na wanafunzi kuhakikisha kuwa utoro haukubaliki Mwanza na kuwa watoto wote wanapaswa kwenda shule.


“Madarasa haya hayatakuwa na maana kama mtoto haendi shule hivyo tuudhibiti utoro sisi wote wanafunzi, wazazi, walimu na walezi wote ni wadau wa kushughulika na suala la utoro”, Alisema CPA Makalla.

Akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mhe Hassan Masala Mkuu wa Wilaya ya Ilemela pamoja na kumshukuru na kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa fedha alizotoa kutekeleza mradi huu amesema kuwa Wilaya ya Ilemela itaanza kuyatumia madarasa hayo mara tu shule zitakapofunguliwa mwezi huu wa tisa 2023.


“Tumekubaliana sisi kama wilaya madarasa haya 54 yaanze kutumika wiki ijayo punde shule zitakapofunguliwa.” Alisema Mhe. Masala


Nae diwani wa kata ya Kahama Mhe.Samwel Buchenja amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kusema kuwa ujio wa shule hii utawezesha mitaa kama mitatu Lukobe,Buteja na Kadinda na kata  ya jirani ya Buswelu kunufaika na ukaribu wa shule hiyo kwa kuondoa adha ya watoto kutembea umbali mrefua kufuata shule.


Akisoma taarifa ya utekelezaji wa mradi wa BOOST, Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilemela Adv. Kibamba Kiomoni amesema kuwa lengo kuu la mradi huu wa BOOST ni kuboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia na kufanikisha upatikanaji wa elimu bora ya awali na msingi sambamba na kupunguza msongamano wa wanafunzi na kuwezesha wanafunzi kukaa kwa uwiano sahihi wa idadi ya wanafunzi katika vyumba vya madarasa.


Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela ilipokea kiasi cha shilingi 1.57 fedha kutoka Serikali Kuu kupitia mradi wa BOOST ambazo zimetumika kujenga vyumba 54 vya madarasa, vyoo matundu 70, majengo 2 ya utawala, ofisi moja ya mwalimu, madawati 1075, viti na meza 90 vya Elimu ya Awali, viti 74 na meza 74 za walimu, na miundombinu ya viwanja vya michezo.

Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.