• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

NAIBU WAZIRI WA UJENZI AKAGUA MIUNDOMBINU ILEMELA

Posted on: January 4th, 2018

NAIBU WAZIRI WA UJENZI AKAGUA MIUNDOMBINU ILEMELA



Naibu Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhe Mhandisi Elias John Kwadikwa amefanya ziara ya kuitembelea halmashauri ya manispaa ya Ilemela ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya ukaguzi wa miradi mbalimbali ya ujenzi wa miundombinu ya barabara inayotekelezwa na Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Mhe Dkt John Magufuli katika halmashauri mbalimbali nchini ikihudhuriwa pia na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya wilaya ya Ilemela, Madiwani wa Manispaa ya Ilemela na Wataalamu wa wakala wa barabara mkoa wa Mwanza TANROADS

Akiwa Ilemela Mhe Naibu Waziri wa Ujenzi amekagua miundombinu ya barabara ya kutoka Sangabuye kupitia Kabusungu kwenda Igogwe, kutembelea kata ya Kayenze kutakapojengwa gati ya Kivuko cha Usafirishaji kwenda Kisiwa cha Bezi, kutembelea daraja la Msumbiji kata ya Kawekamo, kutembelea daraja la Kigala kata ya Buswelu, kutembelea barabara ya Nyamhongolo na barabara ya kutoka Buswelu Kati kwenda Kiwanda cha Coca Cola Nyakato huku akisema kuwa Serikali kupitia Wizara yake itaendelea kuboresha na kuimarisha miundombinu ili kusaidia wananchi sanjari na kupongeza ushirikiano wa viongozi wa wilaya ya Ilemela katika kutatua changamoto za wilaya hiyo hasa katika suala zima la miundombinu na kuwahakikishia kurekebisha changamoto zote za kimiundombinu zilizoelekezwa katika ofisi yake kupitia wakala wa Serikali wa barabara za mijini na vijijini TARURA


‘… Niwashukuru kwa kuwaona kwenye utatuzi wa matatizo mko pamoja na mnashirikiana, niseme tu mheshimiwa mbunge wenu Dkt Angeline Mabula amekuwa akizungumzia sana juu ya ubovu wa barabara za huku mpaka nikapata shauku ya kuja kujionea ili wakati tunazungumzia utatuzi wake wote tuwe kwenye picha moja, Na wenzetu wa TARURA teyari wameshawasilisha barabara zote zenye changamoto na tunazoteyari mkononi na TANROADS pia wapo niwahakikishie tu utoaji huduma kwa wananchi kwetu ni jambo la kipaumbele …’ Alisema


Nae mbunge wa jimbo la Ilemela Mhe Dkt Angeline Mabula mbali na kuomba kuongezwa kwa fedha za mfuko wa barabara amemshukuru Naibu Waziri kwa ziara yake huku akimuomba kuitazama Ilemela kwa jicho la pekee katika suala zima la miundombinu kufuatia upya wake tangu kuanzishwa kwa manispaa hiyo

Meneja wa TARURA wilaya ya Ilemela Mhandisi Fuko Koyoya akisoma taarifa yake kwa niaba ya Mkurugenzi wa manispaa ya Ilemela John Wanga alifafanua juu ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya barabara na madaraja na kuhitimisha kwa changamoto na mpango kazi wa utatuzi wake.

Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.