• Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
    • Malalamiko |
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL
ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government ILEMELA MUNICIPAL COUNCIL

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara na Vitengo
      • Idara
        • RASILIMALI WATU NA UTAWALA
        • MIPANGO NA UFUATILIAJI
        • ELIMU YA AWALI NA MSINGI
        • ELIMU SEKONDARI
        • KILIMO,MIFUGO NA UVUVI
        • VIWANDA, BIASHARA NA UWEKEZAJI
        • MAENDELEO YA JAMII
        • MIUNDOMBINU NA UENDELEZAJI MIJI NA VIJIJI
        • AFYA USTAWI WA JAMII NA HUDUMA ZA LISHE
      • Vitengo
        • USIMAMIZI TAKA NA USAFI WA MAZINGIRA
        • MALIASILI NA UHIFADHI WA MAZINGIRA
        • MICHEZO UTAMADUNI NA SANAA
        • Fedha na Uhasibu
        • SHERIA
        • UKAGUZI WA NDANI
        • MANUNUZI
        • TEHAMA
        • MAWASILIANO SERIKALINI
    • Kata
      • BUGOGWA
      • BUSWELU
        • BUZURUGA
      • BUZURUGA
      • IBUNGILO
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma Zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Leseni
    • Usafi wa Mji
  • Baraza La Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • KAMATI YA FEDHA
      • KAMATI YA MIPANGOMIJI, UJENZI NA MAZINGIRA
      • KAMATI YA HUDUMA ZA UCHUMI, AFYA NA ELIMU
      • KAMATI YA KUDHIBITI UKIMWI
      • KAMATI YA MAADILI YA MADIWANI
      • BODI YA VILEO
      • MFUKO WA KUCHOCHEA MAENDELEO YA JIMBO (CDCF)
      • BODI YA AJIRA
      • ALAT
      • LVRLAC
    • Ratiba ya Mstahiki Meya
  • Miradi
    • Miradi iliyopendekezwa
    • Miradi Inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
    • Sheria Ndogo
    • Majarida
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Umma
    • Hotuba za Viongozi
    • Maktaba ya Picha
    • Video

MWENGE WA UHURU 2023 WALIRIDHISHWA NA MIRADI YA ILEMELA

Posted on: July 14th, 2023

Mwenge wa Uhuru mwaka 2023 ukiongozwa na Ndugu Abdalla Shaib Kaim umeridhishwa na utekelezaji wa miradi yote ambayo imepitiwa na Mwenge wa Uhuru yenye thamani ya fedha kiasi cha Shilingi Bilioni 1.35

Akiongea na hadhara ya wananchi wa Wilaya ya Ilemela katika viwanja vya furahisha, Ndugu Abdalla ameipongeza Ilemela kwa kuwa na miradi mizuri ambayo imezingatia viwango pamoja na thamani ya fedha, huku akisisitiza kuhakikisha kuwa maelekezo yote yaliyotolewa yanafanyiwa kazi.

Awali akizindua barabara za mitaa ya Kirumba (Magomeni,Kabuhoro hadi ziwani zenye urefu wa Km. 0.9 amepongeza kwa mradi mzuri na kuhimiza kuwa barabara itunzwe ili iweze kuwa imara na madhubuti ili iweze kutumika kwa muda mrefu na kwa maslahi mapana ya wana Ilemela na watanzania kwa ujumla


Akiwa katika Shule wa sekondari ya wavulana Bwiru Ndugu Abdalla ameridhishwa na kuipongeza Ilemela kwa namna ambavyo imeweza kuendana na Kauli mbiu ya Mbio za  Mwenge wa Uhuru 2023 isemayo, “ Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya Maji kwa ustawi wa Viumbe hai kwa Uchumi wa Taifa” kwa kupanda miti mingi ikiashiria kuwa Ilemela inaunga jitihada za serikali za  kukabiliana na athari zinazotokana  na mabadiliko ya tabia nchi ambapo amewaongoza wakimbiza Mwenge kitaifa pamoja na viongozi mbalimbali kupanda miti 500.


Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa Wilayani Ilemela umepitia mradi wa udhibiti taka ngumu ambapo Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru Ndugu Abdalla Shaib Kaim, amekabidhi vifaa vya usafi kwa viongozi wa soko la Kiloleli na amewahimiza kuendelea kuunga mkono juhudi zinazoendelea za utunzaji wa mazingira kwa kuhamasisha utunzaji na usafi wa mazingira kuepukana na utupaji wa taka hovyo na matumizi ya plastic.


Akikagua mradi wa vijana wa ufugaji kuku ambao umepatiwa mkopo kiasi cha Shilingi Milioni 15 unaotokana na mapato ya ndani ya Manispaa ya Ilemela, kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru ameipongeza Ilemela kwa kutenga fedha zinazotokana na  mapato ya ndani kwa ajili ya kukopesha makundi ya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu huku akitoa wito kwa vikundi vyote vinavyonufaika na fedha za mikopo kufanya marejesho ili vikundi vingine viweze kunufaika.


Sambamba na hilo Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru 2023 Ndugu Abdalla amezindua jengo la mama na mtoto katika kituo cha afya Buzuruga lililojengwa na fedha za mapato ya ndani kiasi cha shilingi Milioni 199 pamoja na kugawa vyandarua kwa makundi mbalimbali ikiwa ni jitihada za serikali za kutokomeza ugonjwa wa malaria chini ya kauli mbiu isemayo “Ziro Malaria inaanza na mimi;nachukua hatua kuitokomeza”


Halikadhalika Ndugu Abdalla ameutaka uongozi wa Ilemela kuhakikisha ujenzi wa bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum unakamilika kwa wakati na kwa viwango kwa kuzingatia thamani ya fedha ili kuhakikisha dhamira ya serikali ya kuhudumia kundi hili muhimu linatimia, ameyasema haya wakati wa uwekaji wa jiwe la msingi katika ujenzi wa bweni hilo ambalo hadi kukamilika kwake litagharimu kiasi cha shilingi milioni 100 fedha kutoka serikali kuu.


Kwa upande wa Mbunge wa Jimbo la Ilemela, Mhe Angeline Mabula amemshukuru Rais, Mhe Samia Suluhu Hassan kwa kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi kupitia sekta mbalimbali kwani fedha hizo zimetumika katika utatuzi wa changamoto mbalimbali zinazowakumba wananchi wa Ilemela


Mwenge wa Uhuru 2023 umekimbizwa umbali wa Kilometa 57 ukieneza kauli mbiu ya : " Tunza Mazingira, Okoa Vyanzo vya Maji kwa Ustawi wa Viumbe Hai kwa Uchumi wa Taifa." ambapo umezindua miradi miwili, umeweka jiwe la msingi kwenye mradi mmoja na umekagua mradi mmoja.Pamoja na miradi hiyo Mwenge umekagua shughuli saba.

Announcements

  • TANGAZO LA MAOMBI YA MIKOPO YA VIKUNDI VYA WANAWAKE, VIJANA NA WENYE ULEMAVU April 28, 2025
  • TANGAZO MALIPO YA WALENGWA WA MPANGO WA KUNUSURU KAYA MASKINI April 27, 2025
  • TANGAZO LA MWALIKO WA KUHUDHURIA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO WAANDISHI WASAIDIZI KUELEKEA ZOEZI LA UBORESHAJI WA DAFTARI LA KUDUMU AWAMU YA PILI April 27, 2025
  • TANGAZO LA UWEKEZAJI KWA MFUMO WA UBIA (PPP) December 04, 2024
  • Tazama zaidi

Habari mpya

  • WANANCHI 780 WAFIKIWA NA KLINIKI YA HUDUMA ZA MAENDELEO YA JAMII

    May 13, 2025
  • RAI YATOLEWA KWA WAZAZI WENYE WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

    May 05, 2025
  • MKURUGENZI UMMY ASISITIZA HUDUMA BORA ZA AFYA

    April 30, 2025
  • WANANCHI ILEMELA WAHIMIZWA KUHAKIKI TAARIFA ZAO KATIKA DAFTARI LA AWALI LA WAPIGA KURA

    April 30, 2025
  • Tazama zaidi

Video

MAKALA MAALUM MIAKA 3 YA RAIS SAMIA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILEMELA
More Videos

Quick Links

  • Mfumo wa ofisi mtandao
  • Mfumo wa Kieletronikio wa watumishi
  • Mfumo wa TAUSI
  • Vibali vya kutoka nje ya nchi
  • Salary slip

Related Links

  • Tovuti ya Serikali mtandao
  • Tovuti ya Ikulu
  • Tovuti ya utumishi
  • Tovuti ya Tamisemi
  • Tovuti ya Idara ya Habari maelezo
  • Tovuti ya Mkoa wa Mwanza

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

freevisitorcounters's Website

Location Map

Contact Us

    Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela

    Postal Address: 735 MWANZA

    Telephone: + 255 736 200910

    Mobile:

    Email: md@ilemelamc.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • Sitemap

Copyright ©2017 Ilemela Municipal Council . All rights reserved.